• Nairobi
  • Last Updated December 6th, 2023 9:00 PM
Akothee: Msiniulize kuhusu wadhifa wangu wa Rais wa ‘singo matha’

Akothee: Msiniulize kuhusu wadhifa wangu wa Rais wa ‘singo matha’

Na MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI Esther Akoth amewarai wafuasi wake kutomuuliza maswali kuhusu wadhifa wake kama rais wa ‘singo matha’ kwani ameyashuhudia mengi.

Kwenye ujumbe wake, Akothee alisema kuwa njia alizotumia kuhakikisha kuwa wameshirikiana na baba ya watoto wake pia zinafaa kuheshimiwa.

Hali kadhalika, alieleza kuwa licha ya wafuasi wake kumuona kama uhusiano wake na baba ya watoto wake ni mzuri, mengi yamefanyika nyuma.

“Kitambo tufike hapa, jua tu kumekuwa na ‘mapunglu’, ‘mapangla’. Kunao waliojeruhiwa lakini wakawa sawa. Usinifuate kama umeyafumba macho yako,” akaandika kwenye posti aliyojionyesha pamoja na baba ya watoto wake pembeni.

Akothee amekuwa katika mstari wa mbele kupigania masuala ya ‘singo matha’ huku akieleza changamoto anazopitia kama kiongozi wa kundi hilo.

Hapo awali alikuwa amesimulia kuwa alienda kumtembelea bintiye Fancy Makadia na kujua anakoishi lakini muda haukutosha.

Alipoenda kwake, Fancy alikuwa amewaacha vijana wake na kuhuzunika sana alipowaacha.

“Sasa nimeondoka kwake Fancy na ninarudi kwa vijana wangu lakini kumuacha binti yangu peke yake kumenifanya nilie tena. Bado ninashinda nikipigia simu binti zangu wengine Rue Baby na Vesha Lilian ambao wapo Kenya,” akaandika.

Alipoenda kwake Fancy, alibadilisha saa alizokuwa aabiri garimoshi lakini hakumfahamisha baba ya vijana wake ambaye alighadhabika kwa mabadiliko hayo ya saa bila kufahamishwa.

“Baba ya watoto wangu amekasirika ikabidi niabiri basi sababu lazima tule chajio na vijana wangu na amesema kuwa hatanichukua ikipita saa 5:30 kwa sababu lazima awachukue watoto pia,” akasimulia.

 

  • Tags

You can share this post!

Kiongozi wa zamani wa Mungiki mafichoni akisakwa na DCI

Washukiwa saba wanaswa kwenye operesheni dhidi ya pombe...

T L