• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 7:22 PM
Alice Wangui Munyua: Mtaalamu wa afya na mwandishi hodari

Alice Wangui Munyua: Mtaalamu wa afya na mwandishi hodari

NA MAGDALENE WANJA

BI Alice Wangui Munyua alizaliwa katika kijiji cha Gichichi, eneobunge la Othaya katika Kaunti ya Nyeri.

Ndoto yake ilikuwa ni kuwa mwalimu wa somo la Kiingereza kama babake ambaye alimfanya kuvutiwa sana na somo hilo.

“Nilikuwa na ndoto ya kufunza Kiingereza kwani hata katika shule ya upili, nilifanya vyema zaidi katika masomo ya Kiingereza na Bayolojia,” anasema Bi Munyua.

Alipohamia nchini Marekani mnamo mwaka 1987, alijipata akivutiwa na maswala ya afya.

Baada ya muda mfupi, aligundua kuwa alikuwa ameongeza uzani mwingi sana mwilini kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Mnamo mwaka 2012, aliamua kujihusisha na utafiti wa masuala ya kiafya, na aliweza kupoteza kilo 22.6 kwa muda wa chini ya miezi sita.

Aliweza kufikia malengo yake mnamo mwaka 2013, na kulingana na Bi Muyua, hakuna jambo la ziada alilolifanya ili kupunguza uzani huo, ila alifuatia mtindo mwema wa maisha.

“Niligundua kwamba hizi ni njia ambazo zilikuwepo hapo awali katika maisha yangu nilipokuwa nikiishi nchini Kenya. Ni mambo tu ya kiafya ambayo mamangu na nyanyangu waliyafuatilia tangu zamani, ambayo ni pamoja na kula vyakula vyenye afya na kufuatilia afya ya ki akili,” aliongeza.

Alipopata udhamini wa kijiunga na chuo cha kusomea uuguzi, hakusita, na alichukua nafasi hio kujifunza zaidi, kwani tayari alikuwa amevutiwa na sekta hiyo.

Maelezo kuhusu kitabu alichoandika Alice Wangui Munyua, mtaalamu wa afya anayechapisha vitabu vya kuelimisha. PICHA | HISANI

Mnamo mwaka 2015, aliamua kuandika kitabu alichokiita ‘Do like Grandma Did’ ambacho kiliangazia jinsi ya kula vyakula vyenye afya, kama vile bibi au nyanya yake.

Hicho kilifuatiwa na vitabu vingine 10 kuhusu maswala mbalimbali ya kiafya.

Kitabu chake cha hivi punde alichochapisha mnamo mwaka wa 2022, akakipa anwani ‘The Covid-19 Plague’, kimemuwezesha kujibu baadhi ya maswali mengi ambayo huulizwa kuhusu janga la Covid-19.

Jalada la kitabu alichoandika Alice Wangui Munyua, mtaalamu wa afya anayechapisha vitabu vya kuelimisha. PICHA | HISANI

Bi Munyua ana ndoto ya kuchapisha vitabu zaidi kuhusu majanga ambayo huathiri afya ya binadamu.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru Kenyatta atemwa na Jubilee

Mpango kukuza uchumi wa Nairobi kidijitali

T L