• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Bahati akubalika kwa wakwe, matayarisho ya harusi yake na Diana yakinoga

Bahati akubalika kwa wakwe, matayarisho ya harusi yake na Diana yakinoga

NA FRIDAH OKACHI

HARUSI ya mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati na Diana Marua inanukia baada ya wawili hao ‘kupokea baraka’ kutoka kwa babake Diana B, Mzee Omach.

Hii ni baada ya Bahati kutekeleza wajibu muhimu kwa kulipa mahari.

Kupitia mtandao wa Instagram, alithibitisha kwamba alilipa mahari kwa babake Diana.

“Ni rasmi kuwa nimelipa mahari kwa Mzee Omach ambaye ametubariki ili tuendelee na maandalizi ya harusi,” alichapisha Bahati.

Bahati alisema kuwa aliamua kufunga rasmi pingu za maisha na Diana Marua kutokana na kiu ya kutaka kuhalalisha ndoa yao.

Naye Diana alidokeza hakuwa anatarajia kulipiwa mahari tena, kwani msanii huyo alikuwa amefanya hivyo wakati wa maadhimisho ya miaka saba tangu wawili hao kuishi pamoja.

“Hii ni zawadi bora kutoka kwa yule Maulana alinijalia akanipa. Naahidi kufanya kulingana na mafundisho ya Biblia kwa kumpenda na kumheshimu siku zangu zote za maisha,” Diana alirusha ujumbe ulioelekezwa kwa Bahati.

Mzee Omach kupitia video ambayo imekuwa ikisambaa mitandaoni, aliombea wawili hao heri na fanaka katika ndoa yao.

“Naomba muungane nami kuwapa Baraka… Naombea furaha familia ya Bahati kutoka Makueni na familia yetu kutoka Migori,” aliomba Mzee Omach baada ya kupokea mahari jijini Nairobi.

Oktoba 11, 2023, msanii Bahati alichapisha picha ya mkewe Diana akiwa katika maeneo yake ya faragha.

Kilichokuwa cha utata zaidi kuhusu chapisho hilo, ni maelezo mafupi yaliyoambatanishwa kwenye picha iliyomuonyesha Diana akiwa amejilaza kitandani na mtaalam wa usafi akifanya kazi yake huku Bahati akiangalia wazi kilichokuwa kinafanyika.

“Malkia @Diana_Marua aliniambia anataka ‘kusafisha’ kabla nimpe zawadi yake ya kwanza. Kwa sasa hivi tupo @teshisbeautyplace ila nasisistiza niingie pamoja katika chumba cha faragha kuhakikisha,” alichapisha posti hiyo ya kichokozi.

Mnamo Juni 2022, msanii wa muziki wa kufokafoka Diana, alimtaja babake kuwa mzazi aliyemfanya kuwa na nidhamu ya juu.

Mwanamuziki huyo ambaye anafahamika kwa jina Diana B, alisema masharti ya Mzee Omach yalikuwa makali.

Mama huyo wa watoto watatu aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba wakati mwingine alilazimika kutekeleza majukumu ya kuwa ‘mama’ kwa dada zake wawili wadogo.

Kifungua mimba huyo alitekeleza wajibu huo akiwa mwenye umri mdogo, alisema.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Hatua ya Atwoli kuhusu gharama ya maisha...

Kilio cha wahasiriwa wa ubomoaji nyumba Mavoko chageuzwa...

T L