• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Maskini Simba! Afadhali Diamond Platnumz angejua Kizungu

Maskini Simba! Afadhali Diamond Platnumz angejua Kizungu

NA FRIDAH OKACHI

MFALME wa muziki wa Bongo Flava Diamond Platnumz, amewaacha mashabiki na mshangao kwa kuzungumza Kiingereza visivyo akiwa nchini Afrika Kusini.

Diamond ambaye aliachana na Zari Hassan baada ya kujaliwa watoto wawili na mjasiriamali huyo kutoka Uganda, alikuwa amewapeleka wanawe hao katika maskani ya burudani kujivinjari.

Wakati wa kuwarudisha kwenye jumba la kifahari la Pretoria, wanawe hao walisema walihitaji muda zaidi na baba yao.

Binti Tiffah alitaka kufahamu sababu ya babake kutaka kuwaacha mapema na hapo Diamond ambaye anafahamika kama ‘Simba’ akamjibu kuwa anashughulikia wimbo mwingine usiku huo.

“I am going to do another sing (song),” akasema akikusudia kuleta maana ya “naenda kuimba wimbo mwingine”.

Watoto hao wawili walibubujikwa na machozi wakimng’ang’ania baba yao, wakimuomba kuahirisha safari yake.

Msanii huyo alipata wakati mgumu wa kuwatuliza wanawe haswa Nillan.

Mara ya kwanza Diamond kujipata kwenye mitandao akijadiliwa kwa kuboronga Kiingereza ni mwaka wa 2021, wakati wa kipindi cha ‘Young Famous and African’ alipoulizwa umri wake na kusema “I am thirty first” akimaanisha alikuwa na umri wa miaka 31 wakati huo.

Wakati uo huo, mashabiki walimpongeza Bi Zari ambaye ni mama ya watoto hao, kufanikisha mume wake Shabik Lutaaya kukutana na Diamond Platnumz.

Hili likiwa si jambo la kawaida haswa kwa Waafrika. Kwenye video hiyo, Diamond na Shabik walipigana pambaja na kuendelea kuzungumza.

  • Tags

You can share this post!

Wito viongozi wa Mlima Kenya waungane kwa manufaa ya...

Mtego wa EACC wawanasa polisi wawili wakipokea hongo

T L