• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Kero kwa Zuchu Tanasha Donna akimpa Mama Dangote zawadi ya ‘birthday’

Kero kwa Zuchu Tanasha Donna akimpa Mama Dangote zawadi ya ‘birthday’

NA FRIDAH OKACHI

MAMAKE msanii wa jina kubwa Diamond Platnumz, Mama Dangote amepokea zawadi ya manukato na maua kutoka kwa Tanasha Donna ambaye aliwahi kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Tanasha Donna na Diamond walifanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye ni mjukuu wake Mama Dangote.

Juma hili, siku ya Jumatano, Sandra Sanura almaarufu Mama Dangote alitoka kwenye shughuli zake za kila siku na kupata zawadi kutoka kwa Tanasha Donna.

“Duuuh natoka zangu site nakutana na surprise ya zawadi yangu ya birthday kutoka kwa Mama Tom kaka @tanashadonna yaani sina cha kusema ila nasema Alhamdullillah,” Mama Dangote akaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ni jambo ambalo limemkera mno mwanadada anayechukuliwa kuwa mpenzi wa sasa wa Diamond, Zuchu, kiasi cha kuambia wanablogi kwamba hawezi kuzuia ukaribu wa Mondi na ‘ex’ wake huyo Mkenya, kwa sababu “yeye si mume wangu”.

Tanasha Donna alimsherekea aliyekuwa mama mkwe wake huku akimtakia heri njema ya kuzaliwa kwake.

Kwenye mtandao huo wa Instagram, mashabiki wanaomfuatilia walipendezwa na jambo hilo.

Mmoja wa mashabiki aliacha komenti ambayo ilizua mjadala baada ya Mama Dangote kui-pin video hiyo ya zawadi kwenye ukurasa wake, ambapo shabiki huyo alipendekeza Diamond amuoe Tanasha Donna.

Juma lilopita, Mama Dangote alichapisha video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, akionyeshana jinsi Tanasha Donna alivyokuwa nyumbani kwake wakiwa na mtoto Naseeb Junior.

Ikumbukwe Julai 19, 2019, Diamond aliunganisha siku ya kuzaliwa ya mamake mzazi Mama Dangote na Tanasha Donna. Siku hiyo ndiyo Diamond na Tanasha Donna walitangaza kuwa walikuwa wakitarajia kupata mtoto.

Baada ya mtoto kuzaliwa, Mama Dangote alitangaza kwenye mitandao ya kijamii na kuidhinisha kuwa mtoto wa Tanasha alichukua sura yake.

Wawili hao hata hivyo walitengana Juni 2020 kutokana na sababu zao wenyewe, baada ya mtoto Naseeb Junior kuzaliwa.

Tanasha kwenye mitandao yake ya kijamii wakti huo alifuta picha zote ambazo walikuwa pamoja na mkali wa ‘Utanipenda’.

Mengi yamepita tangu wakati huo.

Mnamo Machi 18, 2023, video na picha ya Tanasha Donna akiwa kwake Diamond Platnumz, Dar es Saalam, Tanzania ilionekana ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo alikuwa amempeleka Naseeb Junior kumuona babake ambaye sifa zake zimeenea kote duniani.

  • Tags

You can share this post!

Salasya: Natafuta mwanamke Mzungu wa kuoa

Mwanamume ashtakiwa kwa kumuua mzazi sababu ya...

T L