• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:30 AM
Bernard Wanjohi Njathi: Mwanzilishi wa shirika la kusaidia wafugaji kuweka data muhimu

Bernard Wanjohi Njathi: Mwanzilishi wa shirika la kusaidia wafugaji kuweka data muhimu

Na MAGDALENE WANJA

BERNARD Wanjohi Njathi, 34, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari lakini alipokosa, aliamua kusomea taaluma ya Usimamizi wa Biashara.

“Changamoto kuu katika nchi nyingi barani Afrika ni ukosefu wa rasilimali, jambo ambalo limechangia katika kudidimiza ndoto za wengi,” anasema Wanjohi.

Anaongeza kuwa japokuwa wengi wao ni wakulima, ukosefu wa habari muhimu umesababisha wao kuambulia mapato duni.

Baada ya kufanya kazi katika sekta ya biashara kwa muda wa miaka 12, Wanjohi alihisi kwamba alikuwa tayari kutumia ujuzi huo kutekeleza kufanya miradi mingine na kufanikisha maono yake.

“Nilitaka kutoa suluhisho kwa wafugaji ambao nilishuhudia kuwa walikuwa wakiuza mifugo yao kwa kukosa njia mbadala za kupata pesa za karo, chakula na matibabu,” anaongeza Wanjohi.

Pamoja na marafiki zake, walianzisha shirika la Imfuyo Usajili wakiwa na nia ya kufanya utafiti wa changamoto ambazo wafugaji hupitia.

Bernard Wanjohi Njathi: Mwanzilishi wa shirika la kusaidia wafugaji kuweka data muhimu. PICHA | MAGDALENE WANJA

Kwa muda wa miaka miwili sasa, shirika hilo limekuwa likifanya kazi pamoja na washikadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na ufugaji ili kuwapa wakulima na wafugaji mapato bora kutokana na kuweka data muhimu kuhusu mifugo.

Hao ni pamoja na wataalamu katika sekta za biashara, bima na benki.

Mnamo mwaka 2022, shirika hilo liliweza kupata tuzo mbili kutokana na kazi wanayoifanya wataalamu hao.

“Kwa kutumia teknolojia, pia tumewawezesha wakulima na wafugaji kuweka data muhimu ambazo wanazitumia hata katika kuchukua mikopo ya kujiendeleza,” akasema Wanjohi.

  • Tags

You can share this post!

Akothee: Mume wangu ni moto masuala ya mahaba

Man-City kuvaana na Real Madrid kwenye nusu-fainali ya UEFA...

T L