• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Dadake Betty Kyalo aajiri mtunzi wa watoto wa mbwa wake

Dadake Betty Kyalo aajiri mtunzi wa watoto wa mbwa wake

Na MWANDISHI WETU

DADAKE mdogo mtangazaji tajika Betty Kyallo, Gloria Kyallo alitangaza kuwa na mfanyikazi wa vilebu wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa makala ya pili ya Kyallo Kulture wikendi iliyopita, Gloria alisema kuwa vilebu hao ni watoto wake na sharti waangaliwe vizuri.

Vilebu ni watoto au wana wa mbwa.

Hapo awali, Gloria alikiri mapenzi yake kwa vilebu wake huku akisema yeye hutumia angalau Sh500 kila siku kwa chakula cha vilebu hao; mchele wa Sh200 na nyama ya ng’ombe ya Sh300.

“Nafanya mengi kuhakikisha kuwa vilebu wangu wako sawa. Kwa sasa wapo nyumbani na mfanyikazi wao. Niliwatafutia mfanyikazi kwa sababu vilebu hao ni watoto wangu na wanahitaji mtu kuwashughulikia,” akasema.

Kuzwadi mwana wa mbwa

Julai mwaka jana, Gloria alisherehekea mimba ya kilebu wake na kumzawadi kwa sherehe.

“Hongera mtoto wangu Lulu kwa mimba yako,” akaandika kwenye kurasa zake za kijamii.

Hata hivyo, msichana huyo mwenye umri wa miaka 22 alisema kuwa ana mbwa watatu.

“Mmoja ninaishi naye nyumbani kwangu na hao wengine wawili wanaishi na mamangu Rongai. Unajua dada zangu na mimi tuliondoka nyumbani kwa hivyo mbwa hao humkalisha mamangu lakini naenda kuwaona kila mwezi,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Katibu Esther Ngero ajiuzulu kazi serikalini

Sarakasi za Akothee Ufaransa akizuiwa kutumia majanichai ya...

T L