• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Dj Brownskin akamatwa kwa kusaidia mkewe kujitia kitanzi   

Dj Brownskin akamatwa kwa kusaidia mkewe kujitia kitanzi  

 

NA MERCY KOSKEI

MICHAEL Macharia Njiiri, almaarufu DJ Brownskin, anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani kufuatia kifo cha mkewe, Sharon Njeri, aliyejitoa uhai.

Kukamatwa kwa msanii huyo kunatokana na video iliyofichuka Aprili 2023 na kusambaa mitandaoni ikimuonyesha DJ Brownskin akimrekodi mkewe akinywa sumu nyumbani kwao Garden Estate, Kasarani.

Njiiri alitiwa mbaroni na makachero wa upelelezi wa jinai (DCI) akiwa kwenye klabu kimoja jijini akijiburudisha.

Maafisa wanamchunguza kwa kusaidia mkewe kujiua, kulingana na Kifungu cha 225 (c) cha Kanuni ya Adhabu, kinachosema kuwa, “mtu yeyote anayempata mtu mwingine akijaribu kujiua, au kumshauri mwingine kujiua na hivyo kumshawishi kufanya hivyo; au kumsaidia mtu mwingine kujiua ana hatia na atawajibika kwa kifungo cha maisha.”

Ingawa video hiyo iliibuka mwaka huu, 2023, mke wa DJ Brownskin alifariki Julai 2023.

Kulingana na OCPD wa Kasarani, Anthony Mbogo, DJ Brownskin anazuiliwa katika kituo chake baada ya maafisa kupata agizo la kumzuilia kwa siku saba zaidi huku uchunguzi ukiendelea.

Kulingana na hati ya kiapo iliyowasilishwa mbele ya mahakama siku ya Ijumaa, Juni 2, 2023 iliashiria kuwa Njjeri alifariki kwa kujitoa uhai kupitia usaidizi wa Bw Njiiri.

Wapelelezi walisema kuwa Njiiri alishindwa kumzuia mkewe kutofanya tendo hilo na hivyo kujitoa uhai.

Wapelelezi waliomba siku saba zaidi ili kutafuta wazazi wa marehemu, waweze kuandikisha taarifa  kulingana na tukio hilo na pia kukusanya ushahidi utakaosaidia kumfungulia mashtaka msanii huyo.

  • Tags

You can share this post!

Waziri Kindiki aonya Azimio kuhusu maandamano

Prof Kindiki: Rais Ruto hulala saa zisizozidi tatu,...

T L