• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Erick Omondi na Amber Ray kuporomosha kibao pamoja

Erick Omondi na Amber Ray kuporomosha kibao pamoja

NA MERCY KOSKEI

MCHESHI Erick Omondi na mwanasosholaiti Amber Ray wametangaza kuwa wamejitosa kwenye muziki huku wakitarajia kutoa wimbo wao wa kwanza Ijumaa, Juni 2, 2023.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wawili hao walipeana habari hizo za kusisimua, huku Amber Ray akijitambulisha kama rapa mpya zaidi mjini, na kusema kuwa tofauti yake na wasani wengine ni kuwa hatahitaji mengi ili muziki wake kuvutia.

Eric, kwa upande wake, aliwaahidi mashabiki wake video ya muziki ambayo haijawahi kuonekana akisema kuwa itakuwa mfano kwa wasanii wengine jinsi muziki wa kweli unapaswa kufanywa.

“Ijumaa hii saa 10 alfajiri tutawaonyesha jinsi video ya milioni 3.8 inavyofanana. Tumefanya Wimbo na @iam_amberay ili tu kuonyesha jinsi inavyofanyika…” aliandika.

Ingawa habari hiyo ilikaribishwa vyema na watumiaji wengi wa mitandao, rapa Khaligraph Jones alipinga vikali uamuzi wa Erick na Amber ray.

“You need to pick 1 fight bro ndio tukuchukue serious. Jana ulikuwa unaongoza ajenda muhimu sana iliyonifanya niende studio na kurekodi wimbo unaozungumzia jambo hilo hilo. Kwa mara moja

  • Tags

You can share this post!

Kamene na Bonez washangaza wakidai hutumia mswaki mmoja  

Ntalami aomboleza kifo cha mbwa wake

T L