• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 4:31 PM
Ezekiel Mutua: Mchungaji wako si babako au mamako, komeni upuzi huo

Ezekiel Mutua: Mchungaji wako si babako au mamako, komeni upuzi huo

Na MWANDISHI WETU

AFISA Mkuu Mtendaji Chama cha Wanamuziki Nchini (MCSK) Ezekiel Mutua ameunga mkono kuwa kuwaita viongozi wa kanisa ‘mum’ au ‘dad’ ni kuwadhihaki wazazi halisi.

Bw Mutua alikuwa akirejelea matamshi yake mchungaji Tony Kiamah wa kanisa la KAG River of God, ambaye alikashifu sana uzoefu wa washirika kuwaita wachungaji mama au baba.

“Mchungaji huyo si mamako au babako. Yeye si mzazi wako,” akawaeleza wafuasi wa kanisa lake.

Isitoshe, pasta Kiamah alisema kuwa majukumu ya mzazi huwa hayadadisiwi kwa hivyo unapomwita mchungaji mzazi, kile atakachokueleza ufanye unafanya bila kuuliza maswali.

“Ndio maana watu wengi walifariki huko Shakahola. Huenda viongozi hao walikuwa wakiitwa mama na baba.”

Akimtaja pasta Kiamah kwa kuchimbua mjadala huo, Bw Mutua alisema kuwa matamshi ya mchungaji huyo ni sahihi na mapasta wanaosisitiza kuitwa hivyo huwa na ajenda wanayotaka kuendesha na kuchukua usukani wa wazazi halisi wa mtu.

“Pasta wako hawezi akachukua nafasi au wajibu wa mzazi wako aidha wa kiume au kike. Lazima turekebishe upuzi huu kanisani ili jamii iboreke,” akaandika.

Katika makanisa mengi nchini, wengi wa wafuasi huwaita wachungaji wao mama au baba huku wakiwapa heshima na kutii wanachowaambia.

Licha ya tabia hii kusheheni, udanganyifu unaostawi kwenye makanisa haya huwafanya hata wengine kutotekeleza wajibu wao manyumbani kwao kwa kutekwa na majukumu ya kanisa au kutoogopa kumkosea mchungaji huyo wanayeita mama au baba.

  • Tags

You can share this post!

Wanawake wavamia nyumba na kunyakua mume wa wenyewe

Gachagua – Nilikuwa mlevi kabla kuokoka

T L