• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Fahamu asparaga na faida zake kwa mwili

Fahamu asparaga na faida zake kwa mwili

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MBOGA hii maarufu huja katika rangi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kijani, nyeupe na zambarau.

Inatumika katika milo duniani kote. Asparaga pia ina kalori chache na imejaa vitamini na madini muhimu.

Virutubisho vingi lakini kalori chache

Asparaga ina kalori chache lakini ina sifa ya kuvutia ya virutubisho ikiwa ni pamoja na kalori, protini, mafuta, nyuzinyuzi, vitamini C, A,E na K, folati, potasiamu na fosforasi.

Asparaga pia ina kiasi kidogo cha virutubisho vingine, ikiwa ni pamoja na chuma, zinki na riboflauini. Ni chanzo bora cha vitamini K, kirutubisho muhimu kinachohusika katika kuganda kwa damu na afya ya mifupa.

Kwa kuongezea, asparaga ina folati nyingi, kirutubisho ambacho ni muhimu kwa ujauzito wenye afya na michakato mingi muhimu mwilini, pamoja na ukuaji wa seli na uundaji wa DNA.

Kulinda mwili dhidi ya radikali hatari

Husaidia kulinda seli zako kutokana na madhara ya radikali hatari mwilini.

Mkazo wa oksidi huchangia kuzeeka, kuvimba kwa muda mrefu na magonjwa mengi. Asparaga itasaidia kukabili tatizo hilo.

Kula asparaga pamoja na matunda na mboga nyingine kunaweza kuupa mwili wako aina mbalimbali za vioksidishaji ili kukuza afya njema.

Inaweza kuboresha afya ya usagaji chakula

Nyuzinyuzi ya chakula ni muhimu kwa afya nzuri ya utumbo.Ulaji wa matunda na mboga zenye nyuzinyuzi nyingi unaweza kusaidia kupunguza hatari ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kisukari. Asparaga ina nyuzinyuzi nyingi ambazo haziyeyuki, ambazo husaidia harakati za kawaida za matumbo.

Pia ina kiasi kidogo cha nyuzi mumunyifu, ambazo huyeyuka ndani ya maji na kuunda dutu inayofanana na jeli katika njia ya utumbo.

Kula asparaga kama sehemu ya lishe yenye nyuzinyuzi nyingi ni njia bora ya kukusaidia kukidhi mahitaji yako ya nyuzinyuzi na kuweka mfumo wako wa usagaji chakula kuwa na afya.

Husaidia kutunza mimba yenye afya

Asparaga ni chanzo bora cha folati ambayo pia inajulikana kama vitamini B9.

Folati ni kirutubisho muhimu ambacho husaidia kuunda chembechembe nyekundu za damu na kutoa DNA kwa ukuaji na maendeleo yenye afya. Ni muhimu sana katika hatua za mwanzo za ujauzito ili kuhakikisha ukuaji wa afya wa mtoto.

Husaidia kupunguza shinikizo la damu

Shinikizo la juu la damu huathiri watu wengi duniani kote na ni sababu kuu ya hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Kuongeza ulaji wa potasiamu wakati unapunguza ulaji wa chumvi ni njia nzuri ya kupunguza shinikizo la damu. Potasiamu hupunguza shinikizo la damu kwa njia mbili: kwa kulegeza kuta za mishipa ya damu na kutoa chumvi inayopita kiasi kupitia mkojo.

Inaweza kukusaidia kupunguza uzito

Asparaga inaweza kukusaidia kupunguza uzito.

Ulaji wa vyakula vyenye kalori ya chini na vyenye maji mengi huhusishwa na kupunguza uzito.

Asparaga huwa pia na nyuzinyuzi ambazo zimehusishwa na kupunguza uzito wa mwili.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka keki aina ya Red Velvet

Rigathi atetea ukabila katika uteuzi serikalini

T L