• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:21 PM
Fahamu kwa nini unapaswa kula dengu mara kwa mara

Fahamu kwa nini unapaswa kula dengu mara kwa mara

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MILO inayotokana na mimea inazidi kuwa maarufu huku dengu zikiwa miongoni mwa vyakula hivyo.

Dengu ni mbegu za jamii ya kunde na zipo katika rangi mbalimbali zikiwemo nyekundu, kijani kibichi, kahawia, njano na nyeusi.

Dengu zina nyuzinyuzi nyingi, folati na potasiamu na kuzifanya kuwa chaguo bora kwa moyo na kudhibiti shinikizo la damu na lehemu. Pia ni chanzo cha madini ya chuma na vitamini B1 ambayo husaidia kudumisha mapigo ya moyo.

Inajulikana kuwa dengu zina viwango vya juu vya protini ikilinganishwa na maharagwe.

Hupunguza hatari ya magonjwa fulani sugu

Ulaji wa dengu mara kwa mara unapunguza hatari ya kupata magonjwa sugu kama vile kisukari, unene kupita kiasi, saratani na magonjwa ya moyo. Hii ni kutokana na uwepo wa kinga ya mimea inayoitwa phenoli. Dengu pia zina fenoli.

Kusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Dengu zina nyuzinyuzi ambazo huchangia usagaji chakula na ‘hutia mafuta’ bakteria yenye manufaa ya utumbo ambayo ni muhimu sana kwa afya zetu. Lishe yenye nyuzinyuzi nyingi huhusishwa na faida kadhaa za kiafya ikijumuisha kupunguza hatari ya saratani ya utumbo.

Husaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu

Dengu hupunguza kasi ambayo nishati inayotolewa hutolewa kwenye mkondo wa damu. Hii husaidia kuboresha udhibiti wa sukari ya damu.

Nazo nyuzinyuzi hufanya mtu ajihisi ameshiba sana baada ya kula dengu na hii husaidia kudhibiti hamu ya kula.

Chanzo cha protini ya mmea

Dengu ni chanzo kikubwa cha protini hali inayozifanya kuwa mbadala bora kwa nyama au samaki. Kiasi cha theluthi moja ya kalori kutoka kwa dengu hutoka kwa protini, ambayo hufanya dengu kuwa ya juu katika kiwango cha protini.

Madini ya chuma

Dengu ni mojawapo ya kunde zenye madini mengi zaidi ya chuma. Chuma ni madini ambayo mwili wako unahitaji kutengeneza hemoglobini, protini katika damu ambayo huzungusha oksijeni.

Kuongeza dengu kwenye milo ili kuongeza ulaji wa madini ya chuma kunaweza kusaidia hasa kwa walaji mboga na wasiokula nyama, kwa kuwa wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kupata anemia inayosababishwa na kukosa madini muhimu ya chuma.

  • Tags

You can share this post!

Waiguru alaumiwa kwa kuachilia kampuni ya maji ya Kirinyaga...

MAPISHI KIKWETU: Sambusa za kuku

T L