• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Gachagua asimulia alivyozuru kanisa Kericho nusu ya waumini wakiwa walevi

Gachagua asimulia alivyozuru kanisa Kericho nusu ya waumini wakiwa walevi

NA SAMMY WAWERU

NAIBU wa Rais Rigathi Gachagua amesimulia alivyozuru kanisa moja Kericho na kukuta nusu ya waumini wakiwa walevi chakari.

Bw Gachagua amesema alikuwa ameungana na washirika wa kanisa hilo Bonde la Ufa ambalo hakifichua majina yake, akiwa na kiongozi wa nchi Rais William Ruto.

Naibu Rais alisema ilikuwa jambo la aibu kuona nusu ya washirika walikuwa walevi, hatua iliyoghadhabisha Rais Ruto.

“Ilikuwa aibu kubwa sana mbele ya bosi wangu, Rais William Ruto nusu ya kanisa wakiwa walevi,” Bw Gachagua alisema.

Huku naibu rais akitwikwa jukumu kukabiliana na kero ya pombe haramu na dawa za kulevya na mihadarati nchini, alisema alilemewa kujibu maswali moto na tata ya Rais Ruto.

“Aliniuliza; Ni nani naibu wa rais Kenya? Nikamweleza ni mimi. Alinijibu niwajibike kwa kuzima tabia za aina hiyo,” Gachagua ameelezea.

Jumatatu, Mei 29, 2023 alifanya mkutano Nakuru na viongozi wa kisiasa Bonde la Ufa na wakuu wa polisi eneo hilo ambalo ni ngome ya Dkt Ruto.

“Ni aibu iliyoje Rais na naibu wake hawanywi pombe ilhali maeneo yao vileo na dawa za kulevya zimesheheni?” alihoji.

Mkutano wa Bw Gachagua Nakuru na wadauhusika uliashiria mwanzo wa oparesheni kali dhidi ya pombe haramu Bonde la Ufa na pia dawa za kulevywa na mihadarati.

Kulingana na Bw Gachagua, alipofanya uchunguzi na utafiti kuhusu kukita mizizi kwa unywaji pombe Kericho na Bonde la Ufa, alibaini mengi ya mabaa na maeneo ya burudani yanamilikiwa na wakuu wa askari.

“Itawezekanaje anayetarajiwa atazima pombe haramu ndiye mmiliki wa baa?” Naibu Rais alishangaa.

Alitumia jukwaa la mkutano huo kutoa onyo kali kwa wakuu wa polisi na askari kuhusu oparesheni aliyoanzisha dhidi ya pombe haramu na hatari na dawa za kulevya.

“Kati ya pombe, askari na chifu, lazima mmoja wao aondoke na bila shaka hiyo ni pombe. Ukishindikwa kufanya kazi, tutawapa walio tayari.”

Oparesheni kali kukabiliana na pombe haramu na dawa za kulevya ilianza eneo na Mlima Kenya, Bw Gachagua akiahidi kwamba itaelekezwa kote nchini.

  • Tags

You can share this post!

Hamasisho lapunguza idadi ya wanaofariki wakijifungua...

Dai mganga alishauri washukiwa wafunike Sh700, 000 za wizi...

T L