• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
HUKU USWAHILINI: Kuna jibaba huku limeshindwa kumdekeza mke inavyotakikana

HUKU USWAHILINI: Kuna jibaba huku limeshindwa kumdekeza mke inavyotakikana

NA SIZARINA HAMISI

WANAWAKE wanaoishi Uswahilini, huwa wanavumilia mengi kwenye ndoa zao.

Kwamba wapo wanaoishi na waume zao kama wako mafunzo ya vita.

Mfano ni huyu mwenzetu aliyeolewa na mwanaume mbabe anayejulikana mtaa mzima kwa shari. Huyu mwanaume hafichi na wala hasiti kuonyesha jinsi mfumo dume ulivyomkaa, kiasi kwamba kwake ni kawaida kumwendesha mkewe kwa maneno, kumdhalilisha na kumshushautu wake.

Kawaida mwanamke anapenda kubembelezwa. Apate mwanaume ambaye atamfanya ajisikie au ajione sawa na malkia. Atakapokuwa naye, wazungumze na kupeana michapo sanjari na stori za kuchekesha. Hapo hujiona amefika. Mambo mengine ni ziada kwake.

Lakini huwa tunajionea mengi kwa huyu mbabe wa ndoa huku kwetu. Kwani vitendo vyake huwa havijalishi kama ni mbele ya watu ama la, wakati mwingine humdhalilisha na kumyanyasa mkewe na kumzuia asiongee kitu hata baada ya kumshusha utu wake kwa maneno na pia vitendo.

Juhudi zetu za kuzungumza na huyu mbabe na kumuelimisha kwamba mke sio wa kusemwa semwa na maneno kwani yanaweza kuponda ponda mioyo yao.

Na tumeona matokeo ya moyo kupondeka ni kuyachukia mapenzi, kumchukia mwanaume aliyenaye na uhusiano alionao.

Hali ikishakuwa hivyo, wanawake wa huku kwetu wanayo jinsi ya kukabiliana nayo. Kwani wapo wanaoamua kusaliti ndoa zao kimya kimya na wengine huenda hatua zaidi za kuonyesha masononeko kwa njia mbadala.

Kwamba hawa akina dada wa Uswahilini unapotaka mioyo yao ili waonyeshe upendo wa dhati, hakikisha anakufurahia na anafurahia mapenzi yako kwake kila siku. Ukipotea njia, usimlaumu mtu, kwani atakaa shingo juu, kuangaza yule ambaye anaweza kumfurahisha.

Hapo ni sawa na kuwa njiapanda ya kukusaliti. Kitabaka, sehemu kubwa ya wanawake hupenda kubembelezwa, vilevile mwanaume anyenyekee, kwani hali hiyo humfanya amwone mwenzi wake anajali.

Hakuna kitu ambacho humtesa mwanamke, kama pale ambapo anajiona ameudhiwa lakini mwenzi wake badala ya kuonesha kuguswa, yeye apuuze kisha ajali mambo yake.

Kawaida, bashasha, vicheko na amani ni nguzo muhimu katika uhusiano wa kimapenzi. Humjenga mwanamke kujiona yupo kwenye uhusiano sahihi. Anapovikosa, hudhani anaweza kutafuta penzi lingine. Ni jukumu la kila mwanaume kuhakikisha vitu hivyo vinakuwepo katika uhusiano ili kuufanya udumu.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

JUNGU KUU: Vita vya Uhuru na Ruto kufaidi Raila

UJAUZITO NA UZAZI: Uvimbe ndani ya pua ya mtoto

T L