• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Idadi ya chui yapungua Maasai Mara

Idadi ya chui yapungua Maasai Mara

Na RICHARD MUNGUTI

WAHIFADHI wa Wanyamapori wameeleza masikitiko yao kwa kuendelea kupungua kwa idadi ya chui katika hifadhi ya kitaifa ya Maasai Mara.

Wametaja idadi ya chui imepungua kwa asili mia 31.

Kulingana na ripoti ya data za chui na simba ya taasisi ya Uhifadhi ya Mara Predators (MPCP), kuna Chui 22 waliosalia katika hifadhi kubwa zaidi ulimwenguni.

Ripoti hii ya MPCP ilitayarishwa kati ya Agosti 1 na Oktoba 31, 2022.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo, idadi ya chui imepungua kutoka 32 kutoka 2021.

Ripoti hiyo imesema sababu ya chui au duma kufa mno ni kuwindwa na wawindaji haramu.

Mwaka 2022 kulikuwa na chui 8 wakazaa chengo 22. Chengo ni mtoto wa chui.

Kati yao, chengo 10 walikufa.

Idadi hii ni asilimia 45 ya idadi ya chui walioaga.

Kati ya Shipri 52 waliozaliwa 2021, 18 waliaga na kutimiza asilimia 35 ya chui waliofariki.

Idadi ya chui waliosalia 2022 ilikuwa ni asilimia 42.

Katika kipindi hicho chui 4 waliuawa na wawindaji haram, 3 wakiwa wa kiume na jike moja.

Chui hao wakiume waliouawa¬†walitambuliwa kwa majina Oldarpan, Olarishani na Leboo na jike lililouawa lilikuwa ‘Tano Bora’

Chui aliyekufa kwa sababu asilia alikuwa Entito.

 

 

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Mchicha

Rais Ruto awasilisha jina la Kamau Thugge apigwe msasa...

T L