• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
Jennifer Kananu Mbogori ni mwasisi wa kampuni ya kutengeneza sodo za ubora wa hali ya juu

Jennifer Kananu Mbogori ni mwasisi wa kampuni ya kutengeneza sodo za ubora wa hali ya juu

NA MAGDALENE WANJA

USAFI wakati wa hedhi ni muhimu sana kwa mwanadada au mwanamke yeyote awaye yule. 

Bila shaka ni suala muhimu zaidi la kiafya.

Katika juhudi za kuhakikisha kuwa wanawake hawakabiliwi na wakati mgumu haswa wakati wa hedhi, kampuni nyingi zimezindua taulo za hedhi za aina mbalimbali ila nyingi huwa hazizingatii maswala muhimu.

Baadhi ya taulo hizo huwaathiri sana wanawake, haswa kwa kuwapa maradhi yanayotokana na kutozingatia usafi.

Tukio moja kama hili liliwahi kumkabili Bi Jennifer Kananu Mbogori alipotumia sodo hafifu isiyofaa.

Bi Jennifer Kananu Mbogori akieleza namna ambavyo sodo inafaa kutumiwa. PICHA | MAGDALENE WANJA

Kutokana na hili, Bi Kananu aliamua kufanya utafiti wake binafsi na kutengeneza taulo ambazo zitawafaa wanawake haswa kiafya.

“Katika utafiti wangu, nilishangaa sana kugundua kwamba idadi kubwa ya taulo za hedhi humu nchini zilikuwa zimetengenezwa na kemikali zenye madhara makubwa kwa binadamu. Taulo ambazo zilikuwa zimezingatia afya ya binadamu ni zile tu za kutoka Bara Uropa,” anasema Bi Kananu.

Alichukua hatua akaanzisha kampuni ya kutengeneza sodo kwa jina Dadacare Plus Sanitary Towels. Pamoja na mshirika wake katika biashara, walianza kwa kuwekeza mtaji wa Sh5 milioni pekee.

“Tuliendelea na utafiti na tuligundua kwamba nchi nyingi duniani zilikuwa tayari zimeanza kuzingatia matumizi ya bidhaa salama na wala sio kemikali katika kutengeneza taulo za hedhi,” aliongeza.

Kufikia sasa, kampuni hiyo imeshirikiana na ile ya Via Health ambayo imekuwa kipaumbele katika kuuza bidhaa zilizo salama kwa afya ya akina dada na wanawake kwa ujumla.

“Taulo zetu ni salama sana kwani zinatumia bidhaa kutoka kwa miti na zinazingatia afya ya wanawake,” anaongeza kusema Bi Kananu.

  • Tags

You can share this post!

Waandamanaji wakabiliana jijini Kisumu

Karen Nyamu – Watu wanapendekeza Kituo cha Polisi...

T L