• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Jinsi alivyoanzisha kituo cha michezo kuzuia watoto kuwa waraibu wa simu, vifaabebe

Jinsi alivyoanzisha kituo cha michezo kuzuia watoto kuwa waraibu wa simu, vifaabebe

NA MAGDALENE WANJA

KATIKA maisha ya sasa, watoto wengi wanatumia muda mwingi kwenye vifaa kama vile simu na tarakilishi ambapo wao hucheza michezo ya kila aina mtandaoni.

Mkondo wa maisha umebadilika pakubwa ndiposa Bi Margaret Wachera akaamua kutafuta suluhisho ili kuokoa watoto wake wasiwe waraibu.

Alikuwa hatua hii wakati wa janga la Covid-19, ambapo kulikuwa na zuio la watu kusafiri kama njia mojawapo ya kuzuia au kuounguza kuenea kwa ugonjwa huo.

“Wakati wa janga la Covid-19, mnamo mwaka 2020, nilikaa nyumbani na familia yangu na nikaingiwa na wasiwasi kwani niliona kuwa watoto wangu walikuwa wanazuru mitandao sana,” anasema Wachera.

Aliamua kuanzisha kituo ambacho watoto wangefika hapo na kucheza michezo ya aina mbali mbali na hivyo kuwa mbali na vifaa vya kidijitali.

Margaret Wachera akiwaelekeza watoto wacheze michezo mbalimbali. PICHA | MAGDALENE WANJA

Aliendelea kufanya utafiti wa baadhi ya michezo ambayo angeiongeza kwenye kituo hicho, na baada ya muda mfupi, alipata wateja wengi ambao walikuwa ni watoto wa marafiki na jamaa zake.

Basaye alianza biashara yake rasmi na kukipa jina kituo hicho Funfit.

“Kando na uwanja niliotumia kutoka kipande changu cha ardhi katika eneo la Ruiriu, nilihitaji Sh150,000 za kununua vifaa vya michezo mbalimbali kama vile magwanda ya mchezo wa kuteleza, surupwenye, seti za sanaa, kamba ya kuruka, mipira na swings.

Katika kituo hicho cha michezo, ameweza pia kujumuisha michezo ya watoto wenye aina mbalimbali za ulemavu.

Watoto wanaotembelea kituo hicho hulipa kati ya Sh500 na Sh3000, ambayo hutegemea aina ya michezo .

“Mara kwa mara pia tuna michezo ya wazazi wakati watoto wanapoendelea na michezo yao,” akasema Wachera.

  • Tags

You can share this post!

JIJUE DADA: Kinachosababisha maumivu ya tumbo wakati wa...

Diwani wa Korogocho kujua hatma yake kesho Jumatano

T L