• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Jinsi ya kusafisha na kuzuia vinyweleo kuziba

Jinsi ya kusafisha na kuzuia vinyweleo kuziba

NA MARGARET MAINA

[email protected]

VINYWELEO ni matundu madogo kwenye ngozi ambayo huruhusu mafuta kufikia ngozi.

Wakati mwingine, vinyweleo huziba na mafuta na seli zilizokufa ambazo ngozi hutoa kila siku. Kupitia utunzaji sahihi wa ngozi na matibabu ya ngozi, mtu anaweza kudhibiti au kusafisha vinyweleo zilizoziba.

Tezi kwenye uso hutoa dutu inayoitwa sebamu. Sebamu ni mafuta ya asili kwenye ngozi ili kuziba unyevu. Kazi ya vinyweleo ni kuleta mafuta hayo kwenye uso wa ngozi, ambapo inaweza kulinda na kuimarisha ngozi.

Wakati mwingine, ingawa, sebamu, seli za ngozi zilizokufa, na vitu vingine vinanaswa ndani ya vinyweleo. Tundu lililoziba linaweza kuonekana kuwa kubwa kuliko kawaida.

Wakati mwingine, vinyweleo iliyoziba inaweza kusababisha chunusi.

Mtu anaweza kuchukua hatua kadhaa nyumbani ili kusaidia kusafisha viyweleo zilizoziba.

–         Tumia bidhaa za noncomedogenic

Noncomedogenic inamaanisha kuwa bidhaa haitaziba vinyweleo. Watu wanaweza kutafuta vipodozi, uangalizi wa ngozi na bidhaa za kulinda jua ambazo lebo inazitaja kuwa zisizo na mafuta.

–         Epuka kukuna au kufinya

Baadhi ya watu huona kuwashawishi kukuna, kuchuna, au kusugua vinyweleo vilivyoziba na chunusi. Hii haitasaidia ngozi. Kwa kweli, inaweza kuwafanya kuwa mbaya zaidi kwa kusababisha uharibifu wa ngozi.

–         Kuosha polepole

Kutumia kisafishaji, chenye uwiano wa pH mara mbili kwa siku na maji ya ufuftende (lakini si moto) ni njia isiyodhuru ya kuondoa mafuta ya ziada na seli zilizokufa kwenye ngozi.Ni vyema kuosha uso kwa upole, kwani kusugua kwa nguvu kunaweza kusababisha uwekundu na kuvutia vinyweleo vilivyoziba.

–         Kuchubua

Kuchubua kunahusisha kuondoa seli zilizokufa kutoka kwenye uso wa ngozi. Kufanya hivi kunaweza kusaidia kupunguza umbile la vinyweleo vilivyoziba na, katika hali nyingine, kuzifungua.Kuna aina mbili za kuchubua: kuchubua kwa mitambo, ambayo inahusisha kuondoa ngozi iliyokufa kwa kitambaa au brashi, na utumiaji wa kemikali, ambapo mtu hutumia bidhaa salama ya asidi kuyeyusha uchafu.

–         Retinol

Watu wenye ngozi ya mafuta au ya kuzeeka au vinyweleo kubwa wanaweza kupata kwamba ngozi yao haijanyooka, ambayo inaweza kuchangia vinyweleo kuziba. Kuongeza unyookaji ya ngozi inaweza kusaidia kupunguza kuziba kwa vinyweleo.Retinol ni kiungo cha kutunza ngozi ambacho madaktari wa ngozi hupendekeza kwa watu waliokomaa, wenye ngozi ya mafuta au walio na chunusi.

Ni wazo nzuri kuanza na bidhaa yenye nguvu kidogo na kuitumia kabla ya kulala, kwani retinol wakati mwingine inaweza kusababisha kuwasha kwa ngozi hapo awali.

Unavyoweza kuzuia

Matundu yaliyoziba yana uwezekano mkubwa wa kuathiri baadhi ya makundi ya watu kuliko wengine, lakini unaweza kuchukua hatua kuzuia vinyweleo vilivyoziba kutokea tena kwa:

  • kuweka ngozi safi na yenye unyevu
  • kutumia bidhaa zisizo na mafuta
  • kuosha vipodozi vyote kabla ya kulala
  • kuepuka kugusa uso
  • kutumia mafuta ya kuzuia miale ya jua
  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Uamuzi wa seneti ni funzo kwa magavana, madiwani

Msichana aliyepotea apatikana amefariki nyumbani kwa...

T L