• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 7:22 PM
JUKWAA WAZI: Gachagua, Mutua walumbana kuhusu ‘msaada’ wa Raila kwa Ruto

JUKWAA WAZI: Gachagua, Mutua walumbana kuhusu ‘msaada’ wa Raila kwa Ruto

NA WANDERI KAMAU

JE, viongozi wa Kenya Kwanza wamemwomba kiongozi wa Azimio la Umoja, Bw Raila Odinga, usaidizi wowote kuiendesha serikali?

Jumapili iliyopita, Bw Odinga alidai kuwa hatakubali vishawishi vyovyote kutoka kwa Rais William Ruto kujiunga na serikali yake kumsaidia, kutokana na changamoto zinazoikumba nchi.

Kauli ya Bw Odinga ilionekana kumghadhabisha Naibu Rais Rigathi Gachagua, aliyemjibu Bw Odinga, akimwambia aache kuwahadaa Wakenya, kwani Rais Ruto hajamwomba usaidizi wowote.

Muda mfupi baada ya kutoa kauli hiyo, washirika wa Bw Odinga walimfokea vikali Bw Gachagua, wakidai “hajatosha mboga” kumjibu Bw Odinga.

Baadhi ya watetezi sugu wa Bw Odinga waliojitokeza kumjibu Bw Gachagua ni Profesa Makau Mutua, aliye mshirika wa karibu sana wa ‘Baba.’

Swali ni: Ni nani msema kweli?

Rigathi Gachagua-Naibu Rais

“Bw Odinga anafaa kukoma kuwahadaa Wakenya eti tumemrai kutusaidia kuiendesha serikali. Huo ni uwongo. Hatuwezi kumwambia atusaidie, ilhali yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha kuvurugika kwa mipango ya maendeleo aliyokuwa nayo Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. Hatuwezi kushindwa kufanya kazi wala kutimiza ahadi tulizowaahidi Wakenya.”

Makau Mutua-Mshauri wa Kisiasa wa Raila

“Rigathi Gachagua ni nani kumjibu Bw Odinga? Yeye hajafikia kiwango cha kumjibu hata kidogo. Pili, wao ndio wanaowahadaa Wakenya. Tayari wameanza kumfikia Bw Odinga kuwasaidia kutatua matatizo yanayoikabili nchi kama gharama ya juu ya maisha kwani wameshindwa kuipunguza kama vile walivyoahidi.”

  • Tags

You can share this post!

MIKIMBIO YA SIASA: Ongwae, Ong’era wamtaliki Baba...

JUNGU KUU: Muthama asuka njama mpya dhidi ya Kalonzo

T L