JUKWAA WAZI: Junet, Ichung’wa wakabana koo kuhusu ‘umahsusi’ wa Linturi wizarani
NA WANDERI KAMAU
BILA shaka, ni hitaji la msingi kwa waziri kufahamu majukumu anayofaa kutekekeza katika wizara aliyoteuliwa kuiongoza.
Kwenye shughuli za kuwapiga msasa mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto, Ijumaa, Waziri Mteule wa Kilimo Mithika Linturi alijipata kwenye njiapanda, alipohitajika kueleza mikakati ambayo serikali itatekeleza kuhakikisha kuwa vyakula vilivyotengenezwa kisayansi (GMOs) haviwaathiri Wakenya.
Bi Linturi aliulizwa swali hiyo na mbunge Junet Mohamed (Suna Mashariki).
Baada ya kuonekana kulemewa, Bw Linturi alitetewa vikali na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung’wa, aliyesema kuwa Bw Linturi hawezi kujibu baadhi ya maswali kwani hajaanza kuhudumu kama waziri. Swali lililoibuka ni: Bw Linturi ametosha mboga kuhudumu katika wizara hiyo ama Bw Ichung’wa alikosea kumtetea?
Junet Mohamed-mbunge, Suna Mashariki
“Si Bw Ichung’wah aliyeteuliwa kama Waziri wa Kilimo. Hivyo, lazima amruhusu Bw Linturi kujibu maswali kama anavyoulizwa. Hilo ndilo litatupa picha kamili kuhusu ikiwa ana uwezo wa kutosha kuiongoza wizara hiyo au la. Lazima atufafanulie kuhusu mikakati ambayo serikali itaweka kuwazuia Wakenya kutokana na athari za vyakula vya GMO.”
Kimani Ichungwa-Kiongozi wa Wengi, Bunge
“Bw Linturi bado hajaanza kuhudumu kama Waziri wa Kilimo. Hawezi kujibu baadhi ya maswali, kwani huwa yanategemea sera na mfumo unaowekwa na serikali. Akianza kuhudumu, ndipo atakapoweza kuyajibu. Simtetei dhidi ya maswali, japo huo ndio ukweli.”
Next article
KIGODA CHA PWANI: Wapigakura watarajia makuu kwa...