• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
JUKWAA WAZI: Wandayi na Kamande watofautiana vikali kuhusu hotuba ya Ruto

JUKWAA WAZI: Wandayi na Kamande watofautiana vikali kuhusu hotuba ya Ruto

NA WANDERI KAMAU

Augustine Kamande-mbunge, Roysambu

“Hotuba ya Rais William Ruto ilikuwa ya kipekee. Ilipita matarajio niliyokuwa nayo. Aligusia masuala kadhaa ambayo yamekuwa kero kubwa kwa Wakenya, hasa wale wa kiwango cha chini. Nilifurahishwa sana na hatua yake kurejelea mikakati atakayoweka kutekeleza Hazina ya Hustler, ili kuhakikisha kuwa inamfaa kila Mkenya. Haya ni mapambazuko mapya ya kiutawala nchini ambayo tumekuwa tukiyapigania. Ni mwanzo mpya.”

Opiyo Wandayi-mbunge, Unguja

“Rais Ruto anaonekana kuwa bado yuko kwenye kampeni. Kwake, Kenya inajumuisha watu walioshinda na wale walioshindwa; wale waliomuunga mkono na waliompinga. Hii si kauli anayopaswa kutoa kiongozi anayetarajiwa kuiunganisha nchi. Hotuba hiyo haikuwa tofauti na kauli ambazo alikuwa akitoa wakati wa kampeni. Kando na kurejelea ahadi ambazo amekuwa akitoa, haikueleza mikakati atakayochukua kuhakikisha kuwa zimetimizwa.”

You can share this post!

MIKIMBIO YA SIASA: Raila amempisha Kalonzo kuongoza Azimio...

HUKU USWAHILINI: Ugomvi nyumbani ni burudani mtaa mzima

T L