• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 1:47 PM
Kamene na Bonez washangaza wakidai hutumia mswaki mmoja   

Kamene na Bonez washangaza wakidai hutumia mswaki mmoja  

 

NA MERCY KOSKEI

ALIYEKUWA mtangazaji wa Kiss FM, Kamene Goro na mpenzi wake DJ Bonez wamewaacha wanamitandao kwa mshangao baada ya kufichua kuwa wanatumia mswaki moja.

Mtangazaji huyo wa zamani katika mchezo wa kuulizana maswali kwenye akaunti yake ya Instargam ‘How well do you know your partner alifichua kuwa wanatumia mswaki mmoja na mumewe, jambo ambalo liliwashangaza wengi.

Wanandoa hao walithibitishia wafuasi wao kuwa wao ndio ‘wanandoa kamili’ linapokuja suala la kustareheshana na mapenzi.

La kustaajabisha zaidi, walifichua kuwa wanajisaidia mbele ya kila mmoja kwani hakuna anayeona aibu mbele ya mwingine kwa sababu mapenzi kati yao yamenoga.

Wapenzi hao wawili pia waliarifu wanamitandao kuwa  wanaaminiana kiasi kwamba Kamene au Bonez anaweza kupokea simu na kuzungumza kwa muda mrefu bila kujali ikiwa wanafuatilia mazungumzo.

Kufuatia thibitisho hilo, baadhi ya wafuasi wao walituma jumbe wakiwamiminia sifa kwa upendo wao.

Mwanamitandao kwa jina Eymie_dimpoz alijibu “Aki mapenzi wewe’ huku Lawrencebaba yao akisema kuwa “Mambo imechemukaaa.”

Kamande Mburu alisema “Sioni shida ata boxer na undies we do share tunapendan , life is too short make yourself happy with the one who loves you.”

 

  • Tags

You can share this post!

Utata wa kesi ya mvulana wa miaka 13 akinajisi msichana wa...

Erick Omondi na Amber Ray kuporomosha kibao pamoja

T L