• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 7:55 AM
Kauli ya Wallah: Baada ya mtihani wa shuleni, sasa fahamu kuna mitihani ya maisha duniani!

Kauli ya Wallah: Baada ya mtihani wa shuleni, sasa fahamu kuna mitihani ya maisha duniani!

NA WALLAH BIN WALLAH

KWANZA kabisa niwapongeze wanafunzi wote wapendwa waliovumilia kutumia muda wao wa miaka mingi kusoma shuleni hadi wakafanya mtihani wao wa kuaga darasa la nane pamoja na wote wa sekondari waliokamilisha kidato cha nne. Nyote pongezi na hongera sana!

Sasa kila mmoja wenu ajiulize kwamba baada ya kufanya mtihani wa shuleni na kupewa likizo ndefu tu, utakuwa ukifanya nini kuhusu maisha yako? Au unafanya nini unapokuwa nyumbani kwa sasa? Usisahau huo pia ni mtihani mwingine ambao labda ni muhimu zaidi kuliko mtihani uliofanya shuleni!

Jiulize kwa undani zaidi kwamba baada ya kusoma kwa bidii zote ukafanya mtihani shuleni, je una mtihani mwingine kuhusu maisha yako nyumbani? Je, unaweza kuitumia vipi elimu uliyopata shuleni katika maisha yako na kwa familia yako unapokuwa nao nyumbani?

Binadamu bora, mwenye busara na hekima anapaswa kuwajibika kila wakati kuhusu maisha yake na maisha ya watu wake! Vile ulivyojitahidi kuwajibika ulipokuwa ukisoma shuleni, uendelee vivyo hivyo kuwajibika kuyatekeleza majukumu ya nyumbani. Kuishi si ubwete bali ni mfululizo wa kutekeleza wajibu kwa kufanya kazi na shughuli za kila siku maishani!

Nyumbani si mahali pa kuketi, kuvaa, kula na kulala tu bila kuwasaidia wazazi kuyasukuma maisha kwa kufua, kupika, kulima, kuvuna, kufanya usafi, kuendesha biashara na wewe kuendelea kusomasoma! Hiyo ndiyo mitihani ya maisha duniani!!!

  • Tags

You can share this post!

Jumba la KICC kupigwa mnada serikali ikitafuta pesa za...

Gavana mkaidi atozwa na Seneti faini ya Sh500, 000

T L