• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Madaraka Dei 2023: Rais Ruto aahidi kuzindua bodaboda zinazotumia nguvu za umeme

Madaraka Dei 2023: Rais Ruto aahidi kuzindua bodaboda zinazotumia nguvu za umeme

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto ameahidi kuwa serikali yake inaendeleza mikakati kuleta nchini pikipiki zisizotumia mafuta ya petroli.

Dkt Ruto alisema Alhamisi, Juni 1, akihutubu katika sherehe za maadhimisho ya Madaraka Dei 2023, bodaboda hizo zitakuwa zinatumia nguvu za umeme.

Maadhimisho ya Madaraka Dei 2o23, yalifanyika katika Uwanja wa Moi, Embu ambapo rais aliongoza nchi kusherehekea.

Mkakati aliodokeza, alisema ni miongoni mwa ahadi zake kwa wahudumu wa bodaboda; kuwashushia gharama ya maisha.

“Nimetembea sehemu mbalimbali nchini na kutangamana na wanabodaboda, ninaelewa changamoto zinazowazingira na serikali yangu iko ange kuziangazia.

“Hivi karibuni, tutazindua bodaboda zinazotumia nguvu za umeme ili sekta hii ya uchukuzi iimarike,” Rais alitangaza.

Alisema mkakati huo utakuwa na mpango maalum, kuwezesha wahudumu wa bodaboda kupata pikipiki zinazotumia stima bila vikwazo.

Endapo mpango huo utatimia, utasaidia Kenya kuangazia utoaji wa gesi hatari ya Kaboni ambayo imechangia kero ya mabadiliko ya tabianchi.

  • Tags

You can share this post!

Msitilie shaka Ada ya Ujenzi wa Nyumba, Rais awasihi Wakenya

Madaraka Dei: Viti vingi vyakosa wa kuvikalia uwanjani KMTC...

T L