• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 9:00 AM
Maisha yamenipiga chenga, Baha akiri akigeukia wafuasi wake kumtumia pesa

Maisha yamenipiga chenga, Baha akiri akigeukia wafuasi wake kumtumia pesa

MERCY KOSKEI

MUIGIZAJI wa zamani wa kipindi cha Machachari, Tyler Mbaya almaarufu Baha ameibua wasiwasi baada ya kutangaza kuwa hayuko sawa.

Hii ni baada ya kufichulika kuwa alikopa pesa kutoka kwa watumiaji mbalimbali wa mtandao wa Instagram.

Mwigizaji huyo kupitia akaunti yake makala ya InstaStories, alifunguka kuhusu masaibu yake lakini hakuweka wazi anapambana changamoto anazokumbana nazo.

Pia alitangaza kwamba akaunti zake za mitandao ya kijamii -Instagram na Tiktok zenye wafuasi zaidi ya 760, 000 na 399, 800 mtawalia, zinauzwa.

Mnamo Ijumaa, Juni 2, 2023, mtumiaji wa Instagram aliyetambulika kama Nurse_Judy_ke alifichua mawasiliano ya kisiri baina yake na Baha akimsihi amtumie pesa kwani walikuwa wakikaribia kufukuzwa wanakoishi.

Judy alibaini kuwa baada ya kumtumia Baha pesa mara kadhaa, aliwasiliana na mke wa Baha, Georgina Njenga ambaye alionekana kutofahamu kile mumewe alikuwa akifanya.

Kulingana na Georgina, amekuwa akilipa bili zao zote na kufichua kuwa mumewe huenda akawa mraibu wa kucheza kamari.

“Sijui chochote mnachokisema na pia hatufukuzwi. Baha hakunieleza, kwa sasa ninalipa bili zote kwani amekuwa akipata shida ya pesa lakini hakukopa ili atusaidie kwa lolote pengine kwa manufaa yake. Nasikia vibaya sana anatumia mtoto wetu kupata pesa na kubeti tu,” Georgina alisikitika.

  • Tags

You can share this post!

Prof Kindiki: Rais Ruto hulala saa zisizozidi tatu,...

Waziri Kindiki: Serikali ilichelewa sana kufika Shakahola ...

T L