• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 3:03 PM
MALEZI KIDIJITALI: Likizo ya dijitali hutuliza watoto

MALEZI KIDIJITALI: Likizo ya dijitali hutuliza watoto

URAIBU wa dijitali umelemea baadhi ya watoto na wataalamu wa malezi wanasema ni kawaida enzi hizi za vifaa bebe.

Hata hivyo, wanasema hii haimaanishi waachwe watawaliwe na uraibu huo unaojiri na kuambatana na hatari nyingi zikiwemo za kiafya na kiakili.

Kulingana na mtafiti wa masuala ya watoto na mtaalamu wa malezi dijitali katika shirika la Defend Young Minds, Dkt Lisa Frost, njia moja ya kupumzisha watoto na matumizi au uraibu wa vifaa bebe ni kupitia kuchukua likizo ya kuacha kuvitumia.

Likizo hii, asema Frost, inahusu kuwatenga watoto na vifaa bebe kwa kuviacha nyumbani na kuwapeleka maeneo ya mbali navyo na kuwashirikisha shughuli ambazo hazihusiani na tekinolojia dijitali.

Kwa mfano, utafiti unaonyesha kuwa saa au siku kadhaa nje ya mji bila kuhusika na vifaa vya dijitali kunaimarisha uwezo wa kusoma wa watoto wa kuanzia Gredi ya sita.

“Kupumzisha tekinolojia, kunaongeza nguvu ya uwepo wa hali halisi ya akili ya mtoto,” asema katika tovuti yake ya www.defendyoungminds.com.

Wataalamu wa malezi dijitali wanasema kwamba kupeleka watoto kujivinjari bila vifaa bebe kunawapa fursa ya kupumzisha akili zao na kuelewa hali halisi bila dijitali.

“Inawapa fursa ya kuepuka ushawishi wa kuzama katika mtandao kwa kuwa akili zao zinatekwa na mambo mapya kwa kuwa katika mazingira mapya,” aeleza Frost.

Mtaalamu huyo asema kutenga watoto na dijitali kunawasaidia kupona haraka kutoka dhuluma za mtandao.

Katika kitabu chake kuhusu malezi dijitali kiitwacho, The Glass Between Us, Frost anasema kwamba ili kubaini uhalisia wa binadamu ni muhimu kutafuta njia za kupunguza matumizi ya tekinolojia.

“Kufanya hivi kuna faida kwa afya,” asema.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Kaimati za mboga

Korti yakataa ombi la kukagua kura za ugavana

T L