• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Andaa githeri na uweke bizari na masala ya garam

MAPISHI KIKWETU: Andaa githeri na uweke bizari na masala ya garam

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • vikombe 2 vya mahindi na maharagwe yaliyochemshwa
  • viazi 2 vikubwa vilivyomenya na kukatwa vipandevipande
  • karoti 2 (ziwe cubed)
  • giligilani (majani na shina)
  • pilipili mboga 1 ya kijani iliyokatwa
  • kitunguu maji kilichokatwa
  • nyanya iliyokatwa
  • kijiko ½ pilipili nyeusi
  • kijiko 1 cha garam masala
  • kijiko ½ cha paprika
  • kijiko ½ cha manjano
  • chumvi kwa ladha
  • mafuta ya mboga kwa kukaanga

Maelekezo

Hatua ya kwanza ni kuhakikisha una githeri (mchanganyiko wa mahindi na maharagwe) kilichochemshwa tayari. Unaweza kutumia aina yoyote ya maharagwe.

Weka mafuta na chumvi kwenye sufuria yako. Acha hii ifuatwe na mashina ya dania, vipande vya kitunguu chekundu na pilipili mboga. Harufu itakua nzuri sana katika hatua hii.

Viive kwenye moto mdogo hadi viwe laini na vyenye harufu nzuri kabla ya kuongeza nyanya na viungo.

Ongeza maji kidogo (au mchuzi wa mboga), kisha chemsha kwenye moto mdogo kwa dakika chache. Usikimbilie kuepua kwa sababu viungo vinahitaji kuyeyushwa na mchuzi kuwa mzito.

Unaweza kuweka viazi kwenye githeri ikiwa unapenda. Ongeza viazi na upike kwa muda mchache tu ili viazi visiive kabisa.

Baada ya hayo, ongeza mahindi ya kuchemsha na maharagwe kisha karoti (pia kata vipande vidogo), na kuruhusu kila kitu kichemke kwenye moto mdogo hadi vyote viive. Hii itachukua dakika chache.

Pamba kwa majani ya giligilani iliyokatwakatwa kisha chukua parachichi uongezee ikiwa unapenda. Pakua na ufurahie chakula chako.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi ya kushughulikia tatizo la chunusi za homoni

Jinsi kilimo cha minazi kinavyoimarisha maisha ya wakazi...

T L