• Nairobi
 • Last Updated February 26th, 2024 10:37 AM
MAPISHI KIKWETU: Keki ya kahawa na tufaha

MAPISHI KIKWETU: Keki ya kahawa na tufaha

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 25

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • vikombe 3 unga wa ngano
 • vijiko 2 vya poda ya kuoka
 • kijiko 1 cha chumvi
 • vijiko 2 kahawa
 • kikombe ¼ sukari nyeupe
 • vijiko 2 vya sukari ya kahawia
 • kijiko 1 cha mdalasini
 • vijiko 10 siagi isiyo na chumvi
 • mayai 3 yaliyopigwa
 • kikombe 1 maziwa
 • tufaha 1 la kijani kibichi, likate vipande vipande vya unene wa ¼ inchi.
Keki ya kahawa na tufaha. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Washa ovena hadi joto la nyuzi 200. Paka mafuta kwenye sufuria ya kuokea.

Changanya unga, poda ya kuoka, na chumvi.

Katika bakuli la wastani, piga kwa nguvu pamoja unga, poda ya kuoka, kahawa na chumvi.

Tengeneza sukari ya mdalasini: Katika kijibakuli tofauti, changanya vijiko viwili vya sukari na mdalasini, weka kando.

Piga siagi na sukari, ongeza mayai, ongeza mchanganyiko wa unga na maziwa.

Ukitumia blenda, piga siagi na sukari iliyobaki. Piga mayai hadi yachanganyike. Ongeza mchanganyiko wa unga katika nyongeza tatu, ukibadilisha na maziwa, ukipiga baada ya kila kuongeza mpaka tu kuunganishwa.

Mimina unga kwenye bakuli la kuoka, weka vipande vya tufaha, na sukari ya mdalasini.

Mimina nusu ya unga chini ya bakuli la kuokea. Weka vipande vya tufaha kwenye unga ili vifunike tu unga.

Nyunyuzia mchanganyiko wa mdalasini-sukari kwenye tufaha. Sambaza unga uliobaki juu ya tufaha.

Oka keki kwa muda wa dakika 30-35 au hadi iwe kahawia ya dhahabu na kipimaji au kijiti kikiingizwa katikati kitoke kikiwa safi.

Epua na uiache ipoe kisha pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

Crystal Palace yamtimua kocha Patrick Vieira

BORESHA AFYA: Faida na manufaa ya kula muhogo

T L