• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
MAPISHI KIKWETU: Maini ya kukaanga kwa kitunguu saumu

MAPISHI KIKWETU: Maini ya kukaanga kwa kitunguu saumu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • kilo 1 ya ini la ng’ombe
  • kitunguu maji chekundu kilichokatwa
  • kitunguu maji cheupe kilichokatwa
  • punje 5 za kitunguu saumu
  • kijiko ½ cha zaatari
  • kijiko ½ cha oregano
  • kijiko ½ cha rosemary
  • kijiko 1 cha paprika
  • vijiko 1 ½ vya Royco
  • nyanya 1 iliyokatwa
  • kijiko 1 cha nyanya ya kopo
  • kikombe ½ cha maziwa
  • pilipili mboga iliyokatwa
  • chumvi kwa ladha
  • mafuta ya mboga kwa kukaanga

Maelekezo

Hatua kuu na muhimu zaidi ya kutengeneza ini laini ni kumenya ngozi inayolifunika. Chambua utando kwenye ini na ukatekate.

Loweka kwenye maziwa yako. Utahitaji maziwa takriban kikombe nusu.

Kwa nini tunaloweka ini kwenye maziwa? Tunaloweka kwenye maziwa ili sumu yoyote itoke, na pia, ili kulainisha ini zaidi.

Wacha likae kama dakika 30. Kwa wakati huu, anza na mchuzi.

Katika sufuria, weka vipande vya kitunguu maji, kitunguu saumu na pilipili mboga.

Acha hivi viive hadi viwe laini na vyenye harufu nzuri. Ongeza nyanya, pamoja na nyanya ya kopo. Hakikisha unatumia nyanya iliyoiva vizuri.

Fuatisha na mimea na viungo, kisha robo kikombe cha maji ya moto.

Acha hii ichemke hadi iwe nzito. Mimina maziwa kutoka kwenye ini kabisa kisha ongeza hii kwenye nyanya ili kupika kwenye moto mkali kwa muda wa dakika nane hadi kulainika.

Unapoondoa ngozi, huna haja ya kuchemsha ini. Linakuwa laini sana kulichemsha kabla ya kupika.

Mwagilia kwa juu majani ya giligilani kisha pakua na ufurahie kwa sima au wali.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Mbali na mlo serikali yafaa ikamilishe...

Mbunge wa kale asema jumba ni la Waiguru

T L