NA MARGARET MAINA
UYOGA hujulikana sana kwa ladha yake nzuri na faida za kiafya.
Uyoga pia huwa na vitamini na madini muhimu, na hivyo huongeza ladha kwa mapishi mengi tofauti.
Uyoga huwa na viondoa sumu mwilini.
Uimetambuliwa kwa muda mrefu kama sehemu muhimu ya lishe yoyote na unakuwa na majukumu ya
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa kupika: Dakika 20
Walaji: 2
Vinavyohitajika.
Maelekezo
Katika sufuria juu ya moto wa wastani, ongeza uyoga kwenye safu moja kwa uangalifu ili usijaze sufuria (hii inaweza kuhitajika kufanywa kwa makundi machache kulingana na ukubwa wa sufuria).
Tupia chumvi kiasi juu ya uyoga. Pika bila bila kukoroga wala nini hadi uyoga uanze kutoa unyevu, kama dakika nne hivi. Endelea kupika huku ukichechea, mpaka uyoga uanze kuwa na rangi ya kahawia na unyevu kuvukiza, dakika nane hadi 10.
Ongeza mafuta ya mzeituni kwenye sufuria na endelea kupika huku ukichochea mara kwa mara, mpaka uyoga uchukue mafuta na ugeuke na kuwa na rangi ya dhahabu, kama dakika tatu zaidi. Kisha hamisha uyoga kwenye sahani.
Katika sufuria nyingine juu ya moto wa kati yeyusha siagi. Ongeza vitunguu na pika, chochea, hadi iwe na harufu nzuri kama dakika 2. Nyunyiza unga wa ngano, pika ukichochea, mpaka siagi ichanganyike na unga kwa dakika nyingine mbili.
Polepole sana mwagilia mchuzi, ukikoroga, mpaka mchuzi huo uwe mzito. Sasa ongeza zaatari, sosi ya soya, chumvi iliyobaki nusu ya kijiko, pilipili na uyoga pamoja na juisi yoyote iliyokusanyika.
Koroga uchanganye na kupika hadi mchuzi uwe mzito, dakika tano. Ongeza kwenye juisi ya limau na koroga ili kuchanganya.
Pakua mlo ukiwa moto na ufurahie kwa viazi vilivyopondwa, nyama au chochote ukipendacho.