• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
MAPISHI KIKWETU: Pasta ya kuku yenye krimu na uyoga

MAPISHI KIKWETU: Pasta ya kuku yenye krimu na uyoga

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 1

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • pakiti 1 ya pasta
  • vikombe 2 vya nyama ya kuku iliyosagwa
  • vikombe 2 vya uyoga
  • kijiko ½ cha maji ya limau
  • kijiko ½ cha rosemary iliyokatwa
  • punje 5 za kitunguu saumu kilichosagwa
  • kijiko ½ cha Royco
  • kijiko ½ cha pilipili nyeusi
  • vitunguu maji 2 vyeupe vilivyokatwa

Maelekezo

Kupika tambi:

Kwenye sufuria, chemsha maji juu ya moto mwingi.

Ongeza tambi na upike kwa kufuata maagizo yaliyo kwenye kifurushi.

Tambi zikishaiva, mimina maji kwenye sinki, kisha suuza na maji baridi ya bomba hadi iwe baridi kabisa.

Katika sufuria nyingine, ongeza rosemary yako, vitunguu maji, vitunguu saumu na chumvi. Vitunguu vyeupe vile vina ladha ya hila zaidi ikilinganishwa na vitunguu nyekundu.

Mara baada zikiwa na harufu nzuri, ongeza mipira ya nyama ya kuku pamoja na Royco, pilipili nyeusi na maji ya limau.

Ikiwa huna nyama ya kusaga, unaweza kutumia nyama ya kuku isiyo na mifupa uvikate vipande vipande.

Kabla ya kuongeza Royco na pilipili nyeusi, changanya pamoja kwenye kikombe hadi zitengeneze kibandiko chepesi ambacho utamimina kwenye sufuria yako. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa inasambazwa sawasawa.

Acha hii iive kwa takriban dakika tano kisha ongeza krimu ya kupikia na uyoga. Acha hii ibaki kwenye moto kwa angalau dakika nne ili kila ladha iyeyuke na kuchanganyika kwenye mchuzi wa krimu.

Ongezea pasta yako kwenye mchanganyiko wa mchuzi wa kuku na uyoga, punguza moto, changanya na ufunike kwa dakika tatu kisha epua.

Pakua na ufurahie.

Huwezi kamwe kwenda vibaya na vitunguu saumu na rosemary wakati unatengeneza mlo wowote wa kuku. Uyoga na kuku pia huunganishwa vizuri. Ikiwa huli nyama, unaweza kuandaa sahani hii na uyoga tu na bado utafurahia vile vile.

  • Tags

You can share this post!

Maseneta waitwa kupitisha mswada wa kuteua makamishna wapya...

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa kari ya nyama ya...

T L