• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:20 AM
Mianya tele iliyoko katika soko la nyama na ufugaji

Mianya tele iliyoko katika soko la nyama na ufugaji

NA SAMMY WAWERU

KAMPUNI ya Nema iliyoko kwenye mtandao wa uuzaji nyama, inataja sekta ya ufugaji kama yenye manufaa chungu nzima kuboresha uchumi wa taifa.

Ikiwa katika mtandao huo tangu 2015, mwaka ambao ilianzishwa, inauza ng’ambo asilimia 70 ya nyama inazochinja.

Kulingana na Meneja wa Mikakati, Francis Waweru kampuni hiyo imefanikiwa kuteka soko lenye ushindani mkuu nchi za Mashariki ya Kati Uarabuni.

“Nchi ya Qatar ndiyo pekee hatuuzi bidhaa zetu,” asema afisa huyo.

Ina kichinjio eneo la Ruaraka, Nairobi na imeegemea katika nyama za kondoo kuteka soko nje ya nchi.

Asilimia 30 inayosalia kuunda asilimia mia kwa mia, Waweru anaambia Akilimali Dijitali kwamba inalenga soko la ndani kwa ndani.

Anadokeza kwamba Nema Livestock and Slaughtering Investment Ltd, huuza nyama mbichi na zilizoongezwa thamani (processed).

Kuteka soko lenye ushindani mkuu, kampuni hiyo inaegemea kwa viungo maalum (prime meat cuts).

Mbali na kuuza bidhaa ng’ambo, hupata oda kutoka Ikulu ya Rais hapa nchini.

“Tulianza kusambazia Ikulu nyama miaka minne iliyopita,” Waweru afichua.

Masoko mengine ni taasisi kama vile shule, vyuo, hospitali, hoteli na mikahawa.

Kichinjioni, huondoa mifupa na kutawanya nyama kwa mujibu wa sehemu na viungo maalum.

Kampuni hiyo aidha, ina kandarasi na wasambazaji wa ng’ombe, kondoo na mbuzi.

Hutoa mifugo kutoka Kaskazini Mashariki mwa nchi na Bonde la Ufa, Waweru akisisitiza kwamba waliotwikwa jukumu wamepigwa msasa na kuidhinishwa baada ya kuafikia viwango faafu vilivyowekwa na kampuni hiyo.

“Mifugo tunayosambaziwa lazima iwe huru dhidi ya magonjwa na vimelea,” asisitiza.

Kimsingi, wanatolewa maeneo salama na lazima nyama ziafikiwe kiwango cha kimataifa.

Isitoshe, lazima wawe wanene, wenye afya bora na wa kuvutia.

“Ninahimiza washirika katika sekta ya ufugaji tutilie maanani sekta hii yenye manufaa na mapato chungu nzima.

“Tujizalishie mifugo wenye nyama zenye ushindani mkuu sokoni – ndani na nje ya nchi,” akashauri wakati wa mahojiano.

Kampuni hiyo ni miongoni mwa mashirika na wahusika walioshiriki Maonyesho ya Nyama 2023, katika ukumbi wa KICC, Nairobi.

 

  • Tags

You can share this post!

Ukizoea kufakamia mapochopocho utasumbuliwa na protini...

Wawili wajeruhiwa Mukuru kwa kupigwa na stima

T L