• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
MIKIMBIO YA SIASA: Kujiuzulu Mwakwere kuumiza Wiper Pwani

MIKIMBIO YA SIASA: Kujiuzulu Mwakwere kuumiza Wiper Pwani

USHAWISHI wa chama cha Wiper unatarajiwa kushuka katika eneo Pwani kufuatia kujiuzulu kwa mwenyekiti wake wa kitaifa Chirau Ali Mwakwere.

Hii ni licha ya viongozi wakuu wa chama hicho kinachoongozwa na Makamu wa Rais wa zamani Stephen Kalonzo Musyoka, kushikilia kuwa chama hicho kinangali “imara sio tu Pwani, bali kote nchini.”

Bw Mwakwere, maarufu kama “Dzipapa” anasema kuwa alijiondoa baada ya kutofuatiana na kiongozi wa chama hicho Kalonzo Musyoka kuhusiana na hatua yake (Kalonzo) kuunga mkono msururu wa mikutano ya hadhara ambayo imeratibiwa kufanywa na muungano wa Azimio kote nchini.

Tayari mikutano miwili ilifanyika mwezi jana katika viwanja vya Kamukunji na Jacaranda jijini Nairobi ambapo vinara wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga waliendeleza madai kuwa muungano huo ulishinda urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Hii ni ni kufuatia ufichuzi ambao ulitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni akielezea jinsi kura za Bw Odinga ziliibiwa haswa katika eneo la Mlima Kenya.

Akitangaza rasmi kujiuzulu kwamba kutoka Wiper mnamo Januari 23, 2023, Bw Mwakwere, 77, alisema hataki kuhusishwa na mikutano ya Azimio iliyodai inalenga kuvuruga amani nchini.

“Siwezi kusalia katika chama ambacho inasababisha vurugu miongoni mwa wananchi. Ukitaja Azimio, usinihesabu kama mojawapo ya wanachama au washirika wake. Ukweli ni kwamba nilijiuzulu mnamo Desemba 25, 20222,” akasema Mwakwere.

Akaongeza: “Ikiwa hao watu (Azimio) wanasaka handisheki kupitia maandamano, ninashauri kwamba wasikubaliwe. La sivyo nitaanzisha uasi kutoka eneo la Wadigo.”

Mwakwere ambaye alihudumu kwa miaka mingi katika Waziri katika serikali zilizopita, aliutaka muungano wa Azimio kuipa serikali ya Rais Ruto nafasi ifanye kazi na itekeleze ahadi ilizotoa kwa Wakenya badala ya kutoa vitisho kila mara ya kuchochea vurugu nchini.

“Muwape nafasi wale walioshinda waongoze. Sio lazima umpende mtu aliye mamlakani. Azimio ikome kuzunguka nchini kupanda mbegu za chuki,” akasema Mbunge huyo wa zamani wa Matuga.

Kauli za Mwakwere zilijiri siku ambayo Bw Odinga, Bw Kalonzo, Bi Karua miongoni mwa nyota wengine wa Azimio kuandaa mkutano mkubwa katika wa Kamukunji ambapo walitangaza kutotambua uhalali wa serikali ya Rais Ruto.

Bw Odinga, na wenzake, hata hivyo, wameshikilia kuwa madai ya mfichuzi, asiyetambuliwa kwamba alishinda uchaguzi wa urais kwa zaidi ya kura milioni mbili dhidi ya Rais Ruto.

Lakini safu hii imebaini kuwa kujiuzulu kwa Bw Mwakwere, kimsingi, kulichochewa na jaribio la chama hicho kubatilisha uteuzi Bw Abubakar Said kuwa Mbunge Maalum katika Bunge la Kitaifa.

Duru katika chama cha Wiper zimeambia jarida la “Jamvi la Siasa” kwamba Bw Mwakwere alitofautiana na Bw Musyoka kuhusu suala hilo. Hali hiyo ilipelekea kucheleweshwa kuapishwa kwa Bw Said baada ya suala hilo kuwasilishwa kortini.

“Bw Mwakwere alikosana na Kalonzo tangu mwaka jana kuhusiana na uteuzi wa Saidi kuwa Mbunge Maalum wa Wiper katika Bunge la Kitaifa. Ilitokea kwamba Kalonzo na wakuu wengine wa Wiper walitaka nafasi hiyo imwendee mtu mwingine lakini Dzipapa akakaa ngumu kwamba Saidi ndiye alipasa kupewa nafasi hiyo. Kesi iliwasilishwa kortini na mrengo wa Mwakwere ukashinda,” akasema Mbunge mmoja wa Wiper ambaye aliomba tulibane jina lake kwa sababu siye msemaji rasmi wa chama hicho.

Seneta wa Makueni Enoch Wambua ameshikilia kuwa kujiondoa kwa Bw Mwakwere hakutakitikisa chama hicho.

“Wiper ingali chama maarufu zaidi sio tu eneo la Pwani bali kote nchini. Kuna viongozi wengi zaidi ambao wanaweza kujaza nafasi yake,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Wolves wang’ata Liverpool na kuendeleza masaibu ya...

Papa ahimiza Rais Kiir, Machar kulinda amani

T L