• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
MIZANI YA HOJA: Ni muhimu kuwa na malengo ya kukuelekeza na kukuhamasisha ili kufaulu katika mtihani wako

MIZANI YA HOJA: Ni muhimu kuwa na malengo ya kukuelekeza na kukuhamasisha ili kufaulu katika mtihani wako

NA WALLAH BIN WALLAH

AGHALABU kila mtu anaposoma shuleni au chuoni dhamira yake kuu huwa ni kujifunza aelimike na ajiandae kufaulu katika mtihani.

Hata hivyo, ni muhimu tuelewe kwamba licha ya kujiandaa kufaulu vizuri kwenye mtihani baada ya kusoma vitabu vingi na kurejelea karatasi nyingi za mitihani iliyopita, ni muhimu pia kuwa na malengo maalumu maishani.

Kuishi vizuri si kufaulu mtihani pekee!

Kila mwanafunzi ajiulize anasoma kwa nini? Analenga kufanya nini baada ya kusoma na kufaulu mtihani? Anataka kutumia elimu yake kufanya kazi gani?

Maswali haya yatamchochea mwanafunzi kutambua umuhimu wa kuwa darasani na kuelewa ubora wa kutia bidii kwenye masomo yake ambayo akiyafuzu vyema atayatumia maishani kuyatekeleza malengo yake aliyojiwekea.

Mwanafunzi anayesoma bila malengo yoyote wala kutarajia atakuwa nani wa kufanya kazi gani maishani baada ya masomo, ajue yuko sawa na msafiri anayejiendea tu shaghalabaghala pasi na kuelewa anakoenda wala anachoenda kufanya huko aendako.

Malengo

Asiyekuwa na malengo hujisomea tu afanye mtihani akamilishe aondoke shuleni aende zake bila kujua atafanya nini wala ataishi vipi baada ya masomo.

Hao ndio wale wasemao, “Nimemaliza shule” bila kujua kwamba labda shule ndiyo imemmaliza na kumaliza pesa za mzazi wake!

Tafadhali tuwe na malengo ili tusome kwa bidii na tumakinike kufanya mtihani vizuri tupate matokeo mema ya kutumia kuyatekeleza malengo yetu maishan.

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Kiswahili ni mhimili mkuu wa mshikamano wa...

NGUVU ZA HOJA: Je, Waswahili wanafaa kufunzwa na kutahiniwa...

T L