• Nairobi
  • Last Updated September 28th, 2023 10:25 PM
Mke wa King Kaka akumbuka alivyolipa bili ya deti ya kwanza na mumewe

Mke wa King Kaka akumbuka alivyolipa bili ya deti ya kwanza na mumewe

Na MWANDISHI WETU

MKE wa mwanamuziki King Kaka, Nana Owiti, amefunguka jinsi alivyolipia bili walipoenda deti yao ya kwanza.

Akisherehekea miaka 12 ya kupatana na mwimbaji huyo wa nyimbo za rapu, Nana alisema kuwa tarehe 23 mwezi Mei, 2011 alipatana na King Kaka na wakabadilishana namba za simu.

Deti yao ya kwanza wapenzi hao walienda kutazama filamu huku wakiagana kuwa atakayeshindwa atalipia deti hiyo.

“Niliona ulivyoshindana na nikajua kuwa nimempata mtu kama mimi lakini siku hiyo nililipia kila kitu (kwa hivyo mnajua aliyeshindwa),” akaandika.

Licha ya kukiri kuwa hiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kutazama muvi kwenye ukumbi wa maonyesho ya sanaa na filamu, Nana anasema kuwa bado anakumbuka kile walichovaa siku hiyo.

“Hiyo ni mojawapo ya siku ninazozipenda sana maishani. Kitabu cha maisha yetu kikaanza siku hiyo. Ninamshukuru Mungu kwa kuhakikisha tumepatana. Wewe ni rafiki yangu, mpenzi wangu, na baba mzuri kwa watoto wetu, Nakupenda King Kaka hadi tukunje mgongo,” akamalizia posti yake na kuambatanisha picha zao miaka hiyo.

Wapenzi hawa wawili wamekuwa kielelezo licha ya kuwa mastaa mtandaoni.

Wameonyesha wafuasi wao kuwa ndoa hudumu kwa kuvumiliana kwenye milima na mabonde ya maisha.

Pamoja wanandoa hawa wana watoto wawili.

 

  • Tags

You can share this post!

Mzozo waendelea kuchacha Jubilee

Mandonga ‘Mtu Kazi’ kusisimua tena Nairobi

T L