• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Mkulima Wangari Kuria ambaye amejizolea lakabu ‘Farmer on Fire’ kutokana na juhudi zake shambani

Mkulima Wangari Kuria ambaye amejizolea lakabu ‘Farmer on Fire’ kutokana na juhudi zake shambani

NA MAGDALENE WANJA

MKULIMA Wangari Kuria anatambulika kwa jina ‘Farmer on Fire’, kutokana na juhudi zake shambani.

Wangari pia huwaelimisha wakulima jinsi ya kuongezea mapato kwa kutumia njia bora za ukulima.

Katika kazi hiyo anayoienzi, amechapisha vitabu ambavyo huwapa mafunzo watu wanaonuia kujihusisha na ukulima.

“Nilizaliwa na kulelewa katika eneo la mashambani katika Kaunti ya Nyandarua, na ukulima ndio ilikuwa shughuli kuu. Hivyo sikuwa na budi kujifunza kazi hiyo muhimu kwa uzalishaji wa chakula,” anasema Wangari.

Wangari anaongeza kuwa alipotoka kijini mnamo mwaka 2010 na akujiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi, alihitimu na kujipata katika ukingo wa kuajiriwa kama ilivyokuwa desturi wakati huo.

“Pia nina cheti cha uzamili katika taaluma ya Usimamizi baada ya kuhitimu na kufuzu katika Chuo Kikuu cha USIU mnamo mwaka 2018,” anaongeza.

Anasema alipoajiriwa, kazi yake ilikuwa nzuri lakini miezi michache baadaye, alipoteza kazi hiyo bila kutarajia na alikabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Mkulima Wangari Kuria. PICHA | MAGDALENE WANJA

Baada ya mafikira mengi, yeye pamoja na familia yake waliamua kuhamia katika shamba lao ambalo walikuwa wamelinunua hapo awali katika eneo la Kitengela ili kupunguza mahitaji.

Punde tu alipowasili huko, alijipata ana nafasi kubwa katika kipande hicho cha ardhi ambako alianza kukuza mboga.

Jirani yake ambaye alikuwa na kipande cha ardhi alichomkubalia kukitumia kukuza mboga zaidi.

Mkulima Wangari Kuria. PICHA | MAGDALENE WANJA

Alichota maji na kuzimwagilia mboga zile kwani ilikuwa sehemu kame.

Alipokuwa akiendelea na ukulima wa mboga, siku moja alialikwa kwenye mafunzo ya ukulima wa uyoga, na hapo ndipo alibadilisha mawazo yake na kuegemea ukulima huo kwa kiwango kikubwa.

“Kwa kwaida, mimi huamka saa tano za usiku ambao ni muda bora zaidi wa kuvuna uyoga. Nina wafanyakazi wawili ambao hunisaidia katika kuvuna,” anaeleza.

Baadaye, Wangari huelekea sokoni mwendo wa saa tisa mapema asubuhi ambapo huwa anapatana ana wanunuzi wa jumla.

Wangari anaongeza kuwa ukulima huo humpa raha zaidi ikilinganishwa na kazi nyingine.

Wangari anatumai kuwa ataweza kukamilisha masomo ya kiwango cha uzamifu kwa muda wa miaka sita ijayo.

  • Tags

You can share this post!

Oparesheni kuokoa mateka zaidi wa pasta Paul Mackenzie

Wa Iria achemka kuambiwa Raila ‘hatakikani’...

T L