• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
NGUVU ZA HOJA: Je, Waswahili wanafaa kufunzwa na kutahiniwa lugha ya Kiswahili?

NGUVU ZA HOJA: Je, Waswahili wanafaa kufunzwa na kutahiniwa lugha ya Kiswahili?

NA PROF IRIBE MWANGI

JUZI nilikuwa napiga gumzo na shangazi yangu mmoja aliyewahi kutembea pwani.

Alinieleza kwamba kuna rafiki yake Mswahili aliyemtajia mambo fulani kuhusu Kiswahili na alitaka kusikia maoni yangu kuhusu masuala husika.

Kwanza, rafiki yake huyo alihisi kwamba si haki kusema kuwa lugha waizungumzayo tangu jadi si “sanifu.” Ukweli ni kwamba kusema kuwa lugha si sanifu si makosa. Haimaanisha kuwa lugha ile si sahihi au haifai. La. Usanifu na usahihi ni mambo tofauti.

Hata lugha zilizoendelea kama Kiingereza zina lahaja sanifu. Lahaja sanifu ni mojawapo tu kati ya zaidi ya lahaja 18 za Kiswahili.

Pili, alieleza sahibu yake huyo kuwa Kiswahili kiitwacho sanifu kimekopwa kutoka Tanzania. Hili pia si sahihi.

Lahaja sanifu haimilikiwi na Tanzania wala Kenya wala nchi nyingine yoyote ile. Kwa hakika, ni muhimu kukumbuka kwamba asili ya Kiswahili ni Kenya.

Tatu, alielezwa kwamba Kiswahili ndiyo lugha asilia ya Pwani na hivyo haina haja kufunzwa lugha nyingine asilia katika eneo hilo. Japo sehemu ya kauli hii ni kweli, Kiswahili si lugha asilia ya pekee Pwani. Kuna lugha nyingi zaidi na kila lugha ina umuhimu na muktadha wake wa matumizi na hivyo ni muhimu zote zieleweke. Kiswahli hakifai “kuua” lugha yoyote.

Hatimaye, alieleza kwamba kwa kuwa Kiswahili ni lugha asili ya Pwani, basi haifai kufunzwa wala kutahiniwa Pwani.
Ni muhimu kukariri kuwa Kiswahili sanifu ni tofauti na lahaja nyingine. Hata Waingereza, Wafaransa, Wachina na wengineo hufunzwa na kutahiniwa lahaja sanifu za lugha zao. Hatimaye, kuna lugha nyingine mbali na Kiswahili Pwani.

  • Tags

You can share this post!

MIZANI YA HOJA: Ni muhimu kuwa na malengo ya kukuelekeza na...

Dalali aachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000

T L