• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Njugush: Kuna wakati nilisafiri nje ya nchi kuwachekesha watu lakini ni watu sita walijitokeza

Njugush: Kuna wakati nilisafiri nje ya nchi kuwachekesha watu lakini ni watu sita walijitokeza

Na MWANDISHI WETU

MCHESHI Timothy Kimani almaarufu Njugush ameeleza uvumilivu na bidii katika safari yake ya ucheshi.

Akizungumza katika mahojiano, Njugush alifunguka kuwa kuna siku aliwahi zuru nje ya nchi kuwatumbuiza watu lakini watu 6 pekee ndio walinunua tikiti zake.

Akikumbuka jinsi shoo hiyo ilivyokuwa, Njugush alisema kuwa ilikuwa kama matumbuizo ya kamati na aliketi akiwatumbuiza.

“Kama niliweza kuwatumbuiza watu hao sita kwa vichekesho, sasa ungenipa watu 20 nitakushukuru sana,” akasema.

Akiwashauri wasikilizaji na wafuasi wake, Njugush aliwaomba kutokufa moyo kwani mema huja baadaye.

“Unaweza kataa kuendelea lakini huenda hapo mbele ndipo mambo yako yatafungukia. Hayo ulipitia kitambo yalikuwa mapito yakukukarabati na kukuwezesha kufurahia unayosherehekea leo,” akaongeza.

Akisimulia maisha yake ya utotoni, Njugush alieleza kuwa kuna siku alitengeneza mpira wa karatasi akaisuka vizuri ili wacheze soka siku iliyofuata lakini babake akamletea mpira wa pumzi.

Njugush ni mojawapo wa wasanii nchini Kenya ambao wamekua kwenye tasnia ya sanaa huku jina lake likitamba sana. Huku nyingi ya video zake zikiangazia maisha na changamoto za Wakenya, Njugush alisifiwa hivi majuzi na rais William Ruto.

Kwenye hotuba yake, Rais Ruto alisema kuwa Njugush na msanii mwenzake Butita wanatengeneza pesa nyingi kuliko mshahara wake kupitia sanaa.

  • Tags

You can share this post!

Ruto na Gachagua: Tutawachukulia hatua kali wabunge...

Ruto aonya wabunge dhidi ya kupinga Mswada wa Fedha

T L