• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Njugush na Wakavinye wafunguka kuhusu kufanya kazi pamoja kama wanandoa

Njugush na Wakavinye wafunguka kuhusu kufanya kazi pamoja kama wanandoa

Na MWANDISHI WETU

WACHESHI Timothy Kimani almaarufu Njugush na mkewe Celestine Ndinda anayejulikana kimsimbo kama Wakavinye wamefunguka jinsi wanavyoweza kufanya kazi pamoja licha ya kuoana.

Kwenye mahojiano yao, wawili hao walikanusha madai kwamba huwa vigumu wanandoa kufanya kazi pamoja pasi kuchoshana.

Wengi huamini kuwa wanandoa wanapokuwa pamoja kwa muda mrefu kazini na pia nyumbani wanaweza dhuru mahusiano yao.

Hata hivyo, Wakavinye alieleza kuwa ni jambo la furaha sana kufanya kazi pamoja na mumewe.

“Hakuna kitu kama nitafika nyumbani niongee na mzee, kila kitu papo hapo mara moja. Mara nyingi tuko pamoja. Tunatoka nyumbani tunaenda kazini tunarudi nyumbani kufanya shughuli za kifamilia. Ni vizuri sana,” akaeleza.

Kwa upande wake, Njugush alisema kuwa uhusiano wao pamoja kutoka wawe chuo kikuu umesaidia sana kuimarisha utendakazi wao.

“Tulikuwa tunafanya kozi moja yeye akiwa nyuma ya kamera lakini alijipata mbele. Sasa kuwa na msingi kama huo tunandoto ambazo tunataka kutimiza kwa hivyo inabidi tufanye kazi pamoja ili kuzitimiza,” akasema.

Akikumbuka walivyoanzisha mahusiano yao, Njugush alieleza kuwa kutoka kitambo wamekuwa marafiki wa chanda na pete na mpenziwe jambo ambalo limerahisisha utendakazi wao.

“Sisi kwanza ni marafiki kabla tuanze kufanya kazi pamoja na hiyo imetusaidia sana kudumu kwenye kazi na mahusiano yetu,” akaeleza.

Njugush alifunga ndoa mnamo 2016 na hata ingawa hawakuwa na uwezo mwingi kifedha, huwa anamshukuru sana mkewe kwa kumvumilia.

Wakavinye alisimama na Njugush tangu wakiwa chuo kikuu walipokuwa bila pesa nyingi huku wakiweza kukuzana hadi walipofikia. Wanandoa hao sasa wanao watoto wawili.

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Covid-19 ilivyogeuza ufugaji nguruwe kuwa kampuni

Viva, Miguna Miguna amsuta Rais Museveni kwa pendekezo...

T L