• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Ntalami aomboleza kifo cha mbwa wake

Ntalami aomboleza kifo cha mbwa wake

NA MERCY KOSKEI

MJASIRIMALI na mwanzilishi wa Marini Naturals, Bi Michelle Ntalami, anaomboleza kifo cha mbwa wake.

Mbwa huyo kwa jina Pixel, anadai alifariki kwa njia tatanishi.

Katika ujumbe mzito wa tanzia kwenye akaunti yake ya Instagram, Jumatano, Mei 31, 2023, Ntalami alieleza huzuni yake na kumtaja Pixel kama “mtoto” wake ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu.

Alisema kuwa Pixel, maarufu kama “Pixie” alimaanisha ulimwengu kwake, kwani alimpata wakati alikuwa anapitia mengi maishani baada ya kuachana na mchumba wake.

Alisema kuwa wakati huo alihitaji kuelekeza mapenzi yake yaliyopotea kwa yeyote ambaye asingemchukulia kama jambo la kawaida na hivyo akampata Pixie.

“Nilikuwa nataka kitu chenye afya ambacho singetumia kumaliza uchungu niliokuwa nao.

“Nilimpa jina  Pixel kwa sababu nilihitaji kuleta mwanga maishani mwangu,” Ntalami alisema.

Hata hiyo, Bi Ntalami alisema kuwa chanzo cha kifo cha Pixel bado hakijafahamika kwani alifariki katika hali ambayo haijajulikana kwa sasa, lakini anatumai ‘Karma’ atawatendea haki waliohusika.

“Licha ya kutafuta majibu kwa siku kadhaa ili kutaka kujua alivyopoteza uhai wake, bado haijabainikaa wazi. Hili linaniuma sana. Lakini ninachoweza kusema kwa sasa, ni kwamba Karma atawalipisha. Nimechagua kumkumbuka Pixie kama mtoto mzuri, kwa upendo wote alionao, na upendo ambao aliunyunyizia ulimwengu huu. Alikuwa mbwa mdogo zaidi, na upendo mkubwa zaidi! Nakupenda Pixel. Asante kwa kuwa rangi yangu ndogo,” alisema.

 

  • Tags

You can share this post!

Erick Omondi na Amber Ray kuporomosha kibao pamoja

Mzee arushwa jela kwa ulaghai wa shamba

T L