• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 8:09 PM
AMINI USIAMINI: Kuna nyoka mwenye pua kama pembe ya kifaru

AMINI USIAMINI: Kuna nyoka mwenye pua kama pembe ya kifaru

NA MWORIA MUCHINA

NYOKA anayeitwa ‘Vietnamese Long-Nosed Snake’, ambaye jina lake la kisayansi ni Gonyosoma boulengeri, ana pua iliyochomoka kama pembe ya kifaru.

Mfano huu wa pua ndio ulisababisha wanasayansi kumpa jina lingine la ‘rhinoceros ratsnake’.

Hata ingawa aina hii ya pua haina kazi ya ziada inafanya kwa nyoka hawa, wanasayansi wanaamini ilitokana na mabadiliko ya maumbile.

Nyoka hawa hula wanyama kama panya na wanapatikana kwenye misitu na nyika karibu na maeneo ya maji au mito.

Kadri wanavyozeeka nyoka hawa ndivyo wanabadilika rangi ya ngozi.

  • Tags

You can share this post!

Kutana na mwanamume anayewasiliana na punda vyema

Raila atafutiwa mfupa

T L