NA MWORIA MUCHINA
‘NILE monitor’ ni mjusi mkubwa ambaye ana meno makali na kucha ndefu.
Mjusi huyu huwinda chochote akipatacho na hula hata mizoga.
Anaweza kuwinda kwenye ardhi, ndani ya maji au hata juu ya miti.
Anafahamika kupigana vita na hata wanyama wakubwa kama mamba.
Ni vigumu sana kumnasa mjusi huyu akiwa hai kwa sababu atapigana vita vikali kujinusuru.