• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 5:30 PM
MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka mkate mtamu wa siagi

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka mkate mtamu wa siagi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa kabla ya kuoka: Saa mbili

Muda wa kuoka: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

Unga wa ngano 1 kilo

Hamira ya chenga vijiko 2

Maziwa kikombe ¼

Maji kikombe ¼

Chumvi kijiko 1 cha chai

Sukari vijiko 3

Siagi vijiko 2

Donge la unga wa mkate. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Chemsha maji kiasi halafu tia maji ya ufufutende kwenye hamira.

Ongeza sukari huku ukikoroga. Acha kwa dakika 15 hadi uone povu.

Weka mchanganyiko wa hamira, maji na sukari kwenye bakuli kubwa. Ongeza hapo maziwa ya moto kiasi, siagi iliyoyeyushwa halafu ongeza unga kidogokidogo huku ukikoroga.

Ukiona unga unaanza kunata, hamishia donge kwenye ubao wa kukandia.

Kanda kwa dakika 10 mpaka uone kwamba unapolibonyeza donge, linajirudisha.

Weka donge kwenye bakuli na ufunike na kitambaa safi. Acha unga huo wa donge uumuke kwa muda wa saa moja.

Baada ya saa moja, toa donge na uliweke kwenye ubao. Chukua msukumio usukume donge lote kisha kunja kama mkate.

Weka donge lenye shepu ya mkate kwenye chombo cha kuokea. Funika tena na acha uumuke tena kwa muda mwingine wa saa moja.

Washa ovena na uacha ipate moto kwa dakika 10 kwa nyuzijoto za 180 katika kipimo cha sentigredi.

Oka mkate kwenye ovena kwa dakika 30.

Toa mkate na ubrashi na siagi iliyoyeyushwa juu ya mkate. Rudisha kwenye ovena kwa muda wa dakika mbili kisha toa.

Mkate upo tayari.

You can share this post!

Warembo waangushana kuona kiongozi wa vijana akiwa na gari

EPL: Chelsea yapiga Spurs kwa mara ya tatu chini ya wiki...

T L