• Nairobi
  • Last Updated September 28th, 2023 10:25 PM
MAPISHI KIKWETU: Miguu ya kuku chakula kitamu sana

MAPISHI KIKWETU: Miguu ya kuku chakula kitamu sana

Na PAULINE ONGAJI

KWA kawaida watu wengi wanapomchinja kuku, miguu yake haijumuishwi kwenye mapishi huku wengi wakiichukulia kuwa uchafu.

Lakini ukweli ni kuwa miguu ya kuku ni chakula pia na iwapo itasafishwa vyema na kuandaliwa kama inavyofaa huenda ukawa mlo wa kutamaniwa.

Fuata mbinu hizi:

>Kitoweo: Miguu 12 ya kuku ambayo imetolewa kucha na magamba, vijiko 3 vya sosi ya soya, vijiko 2 vya mvinyo, vitunguu 3 vya majani, kijiko ½ cha sukari, kipande 1 cha chungwa, kijiko ¼ cha pilipili iliyopondwa, maji lita ½. Changanya viungo vyote kisha upike kwa saa 1 ½ kabla ya kuandaa kitoweo kikiwa moto pamoja na ugali, wali au chapati.

>Kukaanga kwa mafuta: Changanya mvinyo, chumvi, kitunguu saumu na pilipili iliyopondwa pamoja na miguu ya kuku na uache kwa masaa mawili. Ondoa, kisha uziweke kwenye sinia lililotandikwa karatasi ili mafuta yakauke. Tia mafuta ya kukaanga kwenye karai kisha uache yawe moto kabla ya kuitumbukiza na ukaange hadi ibadili rangi na kuwa hudhurungi. Andaa na kachumbari pamoja na mchuzi na ugali, wali au chapati.

> Supu: Ichanganye na kilo 1 pamoja na vitunguu vilivyokatwa kwa vipande vikubwa, nyanya zilizoachwa zikiwa nzima, chumvi, pilipili tamu iliyokatwa kwa vipande vikubwa, vijiko 2 vya mvinyo, vijiko 2 vya chai vya mafuta ya mzeituni na maji lita 3 kisha uchemshe kwa saa moja unusu kabla ya kuandaa supu na wali, ugali au chapati.

You can share this post!

HUKU USWAHILINI: Wema kupitiliza utapikiwa majungu

Ripoti yaonyesha watu 43 ‘walipotezwa’ kipindi...

T L