• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 5:50 AM
PATA USHAURI WA DKT FLO: Nahisi maumivu kila ninapoenda haja kubwa, tatizo ni nini?

PATA USHAURI WA DKT FLO: Nahisi maumivu kila ninapoenda haja kubwa, tatizo ni nini?

Mpendwa Daktari,

Kwa majuma kadhaa nimekuwaa nikikumbwa na maumivu kwenye tupu ya nyuma hasa kila ninapoenda haja kubwa. Haya ni maradhi yapi?

Arthur, Nairobi

Mpendwa Arthur,

Kuna mambo kadha wa kadha yanayoweza sababisha shida hii.

Sababu hizi ni pamoja na jeraha kwenye tupu ya nyuma (anal fissure), hali inayotokea hasa mhusika anapoenda choo kikubwa au kigumu.

Hali hii yaweza sababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu kwenye sehemu ya tupu ya nyuma, nasuri ya tupu ya nyuma, misuli kujivuta, jeraha, maambukizi, kuendesha, kidonda au kansa.

Itakubidi umuone daktari ili ufanyiwe uchunguzi wa kina. Tiba hutegemea na nini hasa kinachosababisha hali hii.

Waweza zuia tumbo kuvimba na kinyesi kuwa kigumu kwa kunywa maji mengi, kula chakula kilicho na kiwango cha juu cha nyuzi kama vile mboga na matunda, kufanya mazoezi na kuwa na ratiba ya kuenda haja kubwa.

Pia, waweza kaa kwenye beseni yenye maji yaliyopashwa moto kwa angaa dakika 20 kila siku ili kusaidia kutuliza tishu iliyojeruhiwa. Pia, kuna vijalizo vya nyuzi ambavyo vyaweza kusaidia kupitisha choo chepesi.

  • Tags

You can share this post!

Washukiwa saba wanaswa kwenye operesheni dhidi ya pombe...

Kioni, Murathe warudishwa katika uongozi wa Jubilee

T L