• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
PENZI LA KIJANJA: Anaweza kukwama kwako na hakupendi

PENZI LA KIJANJA: Anaweza kukwama kwako na hakupendi

NA BENSON MATHEKA

KUWA katika uhusiano hakumaanishi unayeita mpenzi wako anakuchangamkia pia.

Hii ni geni kwa baadhi ya watu lakini huo ndio ukweli wa mambo.

Watu wengi wanachangamka wakifurahia kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na watu ambao hata hawatambui uhusiano wenyewe.

“Kuna watu wengi wanaofurahi kwa kuwa wako katika uhusiano wa kimapenzi lakini wanaodhani ni wapenzi wao wanawachukulia vingine. Unaweza kuwa kwenye uhusiano lakini uwe singo zaidi kuliko wasio na wapenzi,” asema mtaalamu wa mahusiano Ruth Odili.

Hivyo basi, anashauri watu kutojipiga kifua wakianza uhusiano kabla ya kubaini iwapo wanayeita mpenzi wao anahisi kama wao.

“Unaweza kufikiri uko katika uhusiano wa kimapenzi wa dhati na mtu, lakini mtu huyo awe hafikirii kama wewe, hayuko katika uhusiano nawe kabisa,” aeleza Odili na kuongeza kuwa “uhusiano sio showbiz tunazoshuhudia watu wakianika kwenye mitandao. Unakutana na mtu na kwa sababu ya tabasamu na joto ya siku moja unachukua selfie na kuanika kwenye mitandao,” asema.

Tabia hii, aeleza, imekuwa mtindo siku hizi na imefanya watu wengi kuvunjika moyo baada ya ukweli kuwadhihirikia.

Kamau* 26 anasema alikuwa katika uhusiano na kipusa aliyedhani alikuwa akimpenda hadi alipogundua alikuwa akitangaza alikuwa akisaka mpenzi.

“Hebu fikiria kuwa katika uhusiano kwa miaka mitatu ukifikiri umepata mwenzi wa ndoto yako ilhali anaambia watu hana mpenzi,” asikitika Kamau na kuongeza kuwa inasononesha wakati mtu kama huyo anakukwamilia.

Odili anasema kwamba lengo la mtu anayekwamilia mwingine huku anatangaza hana mpenzi huwa ni kumharibia maisha.

“Wako watu wa aina hii na lengo lao la kukwamilia mtu huku wakitangaza wako singo ni kuvuruga maisha yake. Ukigundua mtu ana tabia hiyo jitenge naye mara moja,” asema Odili.

Hata hivyo anasema kinachowafanya watu kuzama katika uhusiano wa aina hii, ni faida wanayopata iwe ni ya mali au kutimiza uchu wao.

“Naweza kusema ni waharibifu kwa kuwa wanachojali ni kutimiza maslahi yao pekee,” asema.

Wanasaikolojia wanasema uhusiano wa aina hii unatokana na ubinafsi.

“Kizazi cha sasa kimejawa na ubinafsi, kinafikiria kujihusu. Unaweka mtu katika uhusiano butu ilhali unapochati na wengine unaambia wewe uko sokoni, unaharibia mtu muda akidhani unawaza kama yeye ilhali mawazo yako na yake ni kama ardhi na mbingu,” asema Frank Owen, mwanasiakolojia wa shirika la Maisha Mema.

  • Tags

You can share this post!

Tundo, Carol Radull wapata kazi Safari Rally, Talanta Hela...

FATAKI: Usitoe huduma za mke wa ndoa kwa dume ambalo wala...

T L