• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 2:24 PM
‘Pulahia’ maisha: Akothee awakumbusha ameoleka akitaja mume wake kuwa hodari wa mahaba 

‘Pulahia’ maisha: Akothee awakumbusha ameoleka akitaja mume wake kuwa hodari wa mahaba 

NA SAMMY WAWERU

SIKU kadha zimepita tangu mwanamuziki Esther Akoth ‘Akothee’ asafiri Uswizi (Switzerland), aliko bwanake Dennis Schweizer,

Akitangaza Mei 19, 2023 kupitia mitandao ya kijamii, Akothee alisema ameenda kufuatia agizo la mumewe maarufu kama ‘Omosh’.

“Kwaherini, @BwOmosh ameagizia mkewe. Ninapenda kuwa kwenye ndoa,” alichapisha katika ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Kilichozua ucheshi zaidi mitandaoni, ni kudai anaenda kutafuta mimba.

“Ninaelekea fungate, mimba hiyo,” alielezea.

Wawili hao walifunga pingu za maisha mnamo Aprili 10, 2023 katika harusi iliyohudhuriwa na baadhi ya watu mashuhuri katika ulingo wa muziki, waigizaji, viongozi wa kisiasa na hata waziri katika serikali ya Rais William Ruto.

Mke wa kinara wa Azimio Bw Raila Odinga, Bi Ida Odinga pia alihudhuria hafla hiyo ya kifahari.

Amekuwa akifahamisha mashabiki wake mitandaoni kwamba daktari wake alimweleza atashika mimba endapo atatulia, kufuatia mipango ya hapa na pale kuandaa harusi.

Alisema aliambiwa anahitaji utulivu ili pate ujauzito.

Akothee alisafiri Uswizi manmo Machi 20, 2023.

Hata ingawa mama huyo wa watoto watano ameonekana kuzuru mmoja wa baba wa wanawe, amekuwa akipakia picha Facebook akionekana kuzama kwenye lindi la mapenzi na mahaba na mumewe Dennis.

Dennis Schweizer ni mzungu.

“Kuolewa na Mzungu mjaluo ni Raha. Wale wa maswali; 1. Wapi Omosh? 2. Mbona hauendi fungate? 3. Machozi yanawabishia hodi. Saa hii najua swali mnalotaka kuuliza…” alielezea katika mojawapo ya chapisho.

Katika chapisho hilo, walikuwa Santorini, Greece wanandoa hao wakionekana kufurahia maisha.

Jumatatu, Mei 29, 2023 Akothee alisema anafurahia ‘kuoa’ rafiki wake wa karibu.

“Tunathibitisha jambo; Upendo unadumu ndani na kati yetu…” aliandika katika Facebook.

Alichapisha picha wakiwa kwenye dimbwi la kuogelea.

“Huyu ndiye mume wangu hasa ikiwa umesahau. Omondi wa 7. Tazama video ya harusi yetu You tube uumie kabisa…” alikumbusha wakosoaji wake Jumanne, Mei 30, 2023, akiandamanisha chapisho na picha ya mumewe.

Wanandoa hao wanatarajiwa kufanya harusi nyingine Uswizi.

  • Tags

You can share this post!

AMINI USIAMINI: Kipepeo anayefahamika kama ‘glasswing...

Haaland alivyoweka rekodi kwa kuibuka Mchezaji Bora na...

T L