• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 3:45 PM
SHANGAZI AKUJIBU: Nilimtumia ‘fare’ akala, nashuku ameniacha

SHANGAZI AKUJIBU: Nilimtumia ‘fare’ akala, nashuku ameniacha

KWAKO shangazi. Nimekuwa na mpenzi kwa miaka mitatu. Wiki mbili zilizopita aliondoka akaniambia anaenda kuwatembelea wazazi wake mashambani. Akiwa huko aliniomba nimtumie nauli lakini hajarudi. Inawezekana kuwa ameniacha?

Kama mpenzi wako alikuwa ameahidi kurudi na hajarudi licha yaw ewe kumtumia nauli, ni lazima ana sababu zake. Labda ameamua kumaliza uhusiano wenu. Kama ana simu, mpigie umuulize sababu ya hatua yake hiyo.

Ni miaka 25 sina mpenzi

Vipi Shangazi? Nina umri wa miaka 25 na sijawahi kuwa na mpenzi. Natamani sana kuwa naye lakini nina tatizo la kutangamana na kuzungumza na wanaume. Nahitaji ushauri wako.

Hali hiyo isikutie hofu sana kwa sababu inatokana na maumbile yako. Kila mtu ameumbwa tofauti na wengine. Lakini baadhi ya maumbile hubadilika jinsi mtu anavyokuwa. Hatimaye woga wa kujumuika na kuzungumza na wanaume utakutoka.

Aonyesha nia ya kunioa ila sipo tayari, nina umri wa miaka 38

Vipi shangazi? Nina umri wa miaka 38 na bado sijapata mpenzi. Kuna mwanamume ambaye ananitaka na yuko tayari kunioa. Lakini nahisi siko tayari kwake ingawa siwezi kuelezea sababu. Nishauri.

Wewe sasa ni mtu mzima na uamuzi kuhusu maisha yako kwa jumla umo mikononi mwako. Kama hujawa tayari kwa mapenzi na ndoa subiri hadi wakati huo utakapofika. Lakini kumbuka kuwa umri wako huo si mdogo na unaweza kuwa kikwazo baadaye.

Salamu shangazi? Nina umri wa miaka 28 na nina mpenzi. Nimegundua nina tatizo kubwa. Juzi mpenzi wangu alinipakulia asali kwa mara ya kwanza nikashindwa kulamba. Nahofia hali hiyo ikitokea tena ataniacha. Nisaidie tafadhali.

Hali yako hiyo si ya kawaida kwa mwanamume mwenye umri mdogo kama wako. Huenda kuna upungufu fulani katika mwili wako ambao unahitaji suluhisho la kimatibabu. Ushauri wangu ni kwamba umuone daktari ili akusaidie.

You can share this post!

Jamii yataka kuweka mikataba na wanasiasa kuhusu ahadi

Urusi kusitisha vita Mariupol kwa muda

T L