• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 5:50 AM
SOKOMOKO WIKI HII: Mbunge wa Mumias Mashariki PK Salasya aona mizungu ya Kizungu bungeni

SOKOMOKO WIKI HII: Mbunge wa Mumias Mashariki PK Salasya aona mizungu ya Kizungu bungeni

NA CHARLES WASONGA

KWA mara nyingine mbunge mmoja aliboronga Kiingereza bungeni wiki hii na kupelekea wenzake na Wakenya mitandaoni kuhoji kiwango chake cha masomo.

Peter Kalerwa Salasya, ambaye ni Mbunge wa Mumias Mashariki, Jumatano aliibua kicheko bungeni alipomrejelea Naibu Spika Gladys Shollei mara si moja kama “Madam Speaker Sir). Katika lugha ya Kiingereza “madam” hutumika kurejelea jinsia ya kike huku “Sir” ikitumika kurejelea jinsia ya kiume.

Katika muktadha wa bunge, ni Spika, naibu wake, na wabunge ambao huwasaidia wawili hao kuendesha vikao, ndio hurejelewa kwa maneno ya heshima, kwa misingi ya jinsia zao.

Lakini akichangia mjadala kuhusu hotuba ambayo Rais William Ruto alitoa bungeni, Alhamisi Septemba 29, Bw Salasya alimrejelea Bi Shollei kama “Madam Speaker Sir”.

Wakati mmoja ilimlazimu Bi Shollei kumkosoa mbunge huyo, anayehudumu muhula kwa kwanza, kwa kumwambia kuwa anafaa kumrejelea kama “madam speaker”.

“Madam Speaker, pole pole ndio nimepata,” Salasya akasema.

Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale ni miongoni mwa wabunge waliomkosoa mbunge huyo mwenye umri mdogo, na aliyechaguliwa kwa tiketi ya chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K).

Baadhi ya masuala ambayo Bw Salasya aliangazia katika mchango wake wa kwanza bungeni ni ukosefu wa umeme katika eneo bunge lake la Mumias Mashariki.

“Nataka mamlaka ya usambazaji umeme mashambani (REREC) kuweka stima katika eneo bunge langu ili akina mama walionichagua kwa wingi waweze kunitazama kwenye runinga nikichangia mijadala bungeni,” akasema.

You can share this post!

Mbappe awapita Messi na Ronaldo orodha ya mastaa wakwasi...

WALIOBOBEA: Karume: Mhimili, rafiki wa dhati wa Mwai Kibaki

T L