• Nairobi
  • Last Updated October 1st, 2023 9:40 PM
Sonia: Chipukizi anayelenga nyayo za Priyank Chopra

Sonia: Chipukizi anayelenga nyayo za Priyank Chopra

Na JOHN KIMWERE

NI msanii anayekuja katika tasnia ya uigizaji anayewachana maprodusa wenye kasumba ya kudumisha hadhi ya wanawake.

Anasema kuwa baadhi yao hubagua waigizaji wanaokuja hulka anayosema kwamba huwavunja moyo moyo wengi.

Ni kati ya waigizaji chipukizi ambao wameamua kuvumisha jukwaa la burudani licha ya kwamba bado hawajapiga hatua kubwa.

Kasamani Ruth Isambo maarufu Sonia ni msanii anayeibukia ambaye ni msomi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Marist International.

Kando na uigizaji ni video vixen, muuzaji wa magari na pia mapambo ya wanawake.

”Kiukweli baadhi yetu hujipata njia panda na kukosa ajira baada ya maprodusa wengi kutoa matakwa sampuli hiyo,” anasema na kuongeza kuwa taifa hili limefurika waigizaji wengi tu wa kike na wanaume lakini tatizo nafasi za ajira ni chache kwa kuzingatia kwamba sekta ya uigizaji haijapiga hatua nchini.

Aziza

Binti huyu alianza kujituma katika masula ya uigizaji mwaka 2018 baada ya kuvutiwa na filamu iitwayo ‘Aziza,’ kazi yake Sanaipei Tande aliye kati ya waigizaji wanaofanya vizuri nchini. Msichana huyu ameshiriki filamu kama ‘Elizeti Series,’ na ‘Invisimble Enemy,’ pia anajivunia kushiriki vipindi tofauti kama Quiz Show (Switch TV) na Perfect Match (Ebru TV) pia I can dance (KTN). Kadhalika kama video vixen ameshiriki nyimbo iitwayo Chogoro. Hata hivyo bado hajafanikiwa kushiriki filamu na kupeperushwa katika runinga jambo analozidi kumwomba Mungu ili afaulu kulitimiza.

Priyank Chopra

Katika tansia ya uigizaji dada huyu analenga kufuata nyayo za kati ya waigizaji mahiri duniani kama Priyank Chopra mzawa wa nchini India. Msanii huyu anajivunia kuigiza filamu kama ‘Baywatch’, ‘Krish, ‘The White Tiger’, na ‘The Matrix 4’ kati ya nyingine.

Pia anataka kujikaza kwa udi na uvumba huku akilenga apate umaarufu, filamu zake zitambulike na aive kutinga kiwango cha Hollywood. Binti huyu pia anatamani sana kushiriki filamu ya Pocher au filamu mpya ya Zora inayopeperushwa kupitia runinga ya Citizen TV.

Aidha anasema angependa sana kufanya kazi na kati ya wasanii wa kike wanaozidi kujituma kiume nchini akiwamo mwigizaji Sarah Hassan ‘Zora,’ ‘Tahidi High,’ na Vera Sidika ‘You Guy’, ‘My Gal’.

Kasamani Ruth Isambo maarufu kama ‘Sonia’. Picha/ John Kimwere

Kimataifa angependa sana kutua jukwaa moja na mwana mitindo maarufu nchini Ufilipino Catriona Gray.

Kadhalika angependa kushiriki mashindano ya urembo nchini hasa kubeba taji la Miss Kenya na Miss World. Anashauri wenzie wasife moyo na wanapopata nafasi ya kuigiza wawe wakijituma bila kulegeza kamba maana hawafahamu ya kesho.

Changamoto

Anasema waigizaji hupitia panda shuka nyingi ikiwamo kufanya kazi na kutolipwa.

”Sina shaka kutaja kuwa produsa wengi hupenda kutushusha hadhi hali ambayo huchangia wengi wetu kukimbia na kuacha uigizaji,” akasema.

Katika mpango mzima kisura huyu anasema kuwa amepania kushiriki filamu anapotamani sana zifanikiwa kupeperushwa kupitia runinga ya Citizen TV na Netflix.

You can share this post!

Marufuku dhidi ya Ngii yabatilishwa, sasa atawakilisha...

Man-City yatoa ofa ya mwisho ya Sh15.6 bilioni kushawishi...